Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_2915.jpg
 
Askari Polisi, twawaombea kwa Mwenyezi Mungu aliye mpweke. Kazi yenu ni ngumu, watanzania wanategemea umuhimu wenu kuwalinda wao wenyewe na mali zao. pambaneni angalau muweze kuwabaini watu wsiojulikana ili taifa lilejee kwenye hali yake. simamieni uadilifu ndani yenu, jiwekeni karibu na uma ili mpate ushirikiano kwa ajili ya ufanisi wa kazi zenu
 
Majaji, Mahakimu na idara nzima ya mahakama. Kwa niaba ya wanauzi huu na watanzania kwa ujumla. Twawaombea kwa Mungu wa Adam, mungu wa Nuhu, mungu wa Ibrahim, Mungu wa Mussa Mungu wa Masihi mwana wa Mariam, Mungu wa Muhammad na Mungu wetu sote, simamieni haki za watanzania kwa weledi, taifa linategemea uwezo wenu ili kila mmoja apate haki yake.
 
Madaktari, senior na junior. Twawaombea kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, akufanyieni wepesi kwenye majukumu yenu, muepuke maambukizi toka kwa wagonjwa wenu, muepuke tamaa ya mali kuliko utu wenu kwa wagonjwa wenu. Twaomba Tangulizeni utu, uzalendo, upole na huruma kwa wagonjwa wa Tanzania na Mungu atawasimamia .
 
Walimu. Nyinyi ni watu MUHIMU kwa maendeleo ya Watanzania, Mwenyezi Mungu mtukufu azidi kuwapa moyo wa subira kwenye majukumu yenu, maana maisha yenu hayafanani na taaluma yenu, lakini tangu zamani mmetanguliza Uzalendo, hekima, busara kwa watoto wa Taifa hili. Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom