Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4d867b10d7b6865802b0491e1c2b18dc.jpg
Toyota
 
5.Ni watu gani muhimu sana kwako? Umepanga kuwafanyia nini ili kuimarisha mahusiano baina yako na wao?
-Thamini watu wote lakini wapende zaidi waliokaribu na wewe katika maisha yako kama vile wazazi, watoto au mpenzi wako. Je umeonyesha kuwa unawajali na kuwapenda? Wakati mwingine huwa tunatingwa na mambo mengi na kusahau watu waliomuhimu kwetu. Kila unapojiuliza swali hili litakufanya uwakumbuke wote waliomujimu kwako. Jijengee mazoea na mahusiano mazuri na washirika wako kwa kushirikiana nao vizuri nao watakupenda.
Maswali haya ni ya msingi sana, kila unapojiuliza na kupata majibu ya maswali haya nina imani yataleta athari ya kimaendeleo katika maisha yako. Jiulize leo hakika mafanikio yatakuwa karibu yako.
 
tumia muda wako leo mchache na jiulize maswali yafuatayo katika maisha yako.

1. Hali ya afya yako ikoje kwa sasa?
Afya yako ndio utajiri namba moja duniani utakaokuwezesha kutimiza malengo yako yote uliyojiwekea hapa duniani. Unakula vizuri vyakula vya kujenga mwili na kuupa mwili kinga dhidi ya magonjwa? Unafanya mazoezi ya mwili? Unapunguza uzito? Unakunywa maji mengi? Unakula matunda? Au unakula vyakula vyepesi vya kuharibu mwili wako kama vile chips na vinywaji kama vile soda.
 
2. Mtazamo wako juu ya maisha yako ukoje kila siku?
Maisha yako unayachuliaje je katika mtazamo chanya au hasi. Maisha yako yametawaliwa na furaha au huzuni? Maisha ni furaha na una uamuzi wa kuchagua kuishi kwa furaha au huzuni bila kujali matatizo uliyokuwa nayo. Kama unaishi maisha yako katika mtazamo chanya ni rahisi kuishi katika furaha na mafanikio lakini ukiishi katika mtazamo hasi lazima utaona maisha ni huzuni badala ya furaha na utakuwa mlalamikaji na mtu wa kulaumu.
 
3. Mahusiano yako kiujumla katika idara hizi zifuatazo yako?
i. Mahusiano yako na familia yako ya koje? Mara ya mwisho ni lini ulimwambia au uliwaambia watoto wako kuwa unawapenda au nakupenda? Mara ya mwisho ni lini uliwakumbatia na kuwabusu watoto wako? Watoto wanahitaji upendo na kuhisi kuthaminiwa je watoto wako au katika familia yako wanaonja falsafa ya tunda la upendo? Au umeshakufa siku nyingi katika mioyo ya watoto wako wanakusubiri tu wakuzike? Unapata muda wa kukaa na familia yako?
 
ii. Mahusiano yako na mpenzi au mwenza wako yakoje? Falsafa ya upendo ipo? Uaminifu, kuvumiliana, furaha , amani ipo katika mahusiano yenu? Kama ipo au hakuna unachukua hatua gani kurekebisha hiyo hali? Vuta picha ya nyuma mlivyokutana wakati mko katika uchumba jinsi ulivyokuwa unaonesha upendo na kujali ni sawa na sasa? Kama siyo nani ni kiini cha kosa na umechukua hatua gani baada ya kujua kama wewe au yeye ndio kiini cha kosa kinachowafanya mwendelee kuishi maisha ambayo hayastahili kuishi kama wapenzi?
 
iii. Mahusiano yako ya koje na marafiki wako, ndugu, jamaa na jirani zako? Umekuwa ni faraja au kikwazo kwa watu hawa wa karibu kwako? Marafiki zako na watu waliokuzunguka wananufaikaje na wewe, wanajifunza nini kutoka kwako au wewe ndio umegeuka kuwa adui wa kurusha makombora ya kusengenya, umbea, wivu, chuki na kutokusamehe na kulipa visasi? Jitafakari leo na uchukue hatua chanya.
 
4. Ni kwa namna gani unailisha akili yako chakula?
Unatakiwa kuilisha chakula akili yako na chakula cha akili au ubongo wako ni maarifa na siyo kitu kingine. Jiulize katika taaluma uliyosomea umeshasoma vitabu vingapi vya kuongeza maarifa tofauti tofauti na vitabu vya darasani yaani ambavyo haviko katika mtaala wa darasani? Tokea umalize shule au chuo ni mara ngapi umesoma kitabu kwa ajili ya kuona akili yako?
 
5 .Maisha yako yana msaada kwa watu wengine?
Unaishi maisha ya kushawishi watu au unaishi maisha ya kugeuka kuwa mwalimu mzuri wa kukosoa na kukatisha tamaa watu au unaishi maisha ya kuwaaminisha watu kuwa mambo yanawezekana kama mtu akiamua kuchukua hatua. Jiulize swali hili leo.
 
Ni mara ngapi unasoma makala chanya za kujenga na kusikiliza sauti zilizorekodiwa za watu makini duniani? Au wewe ndio unakomaa na kufuatilia udaku katika magazeti, mitandao ya kijamii kujua Fulani kafanya nini na mengine mengi je unafikiri hiyo ndio njia ya kuongeza maarifa kwa fuatilia udaku? Soma vitabu rafiki na jifunze kwa watu utalisha ubongo wako maarifa mapya kila siku.
 
Back
Top Bottom