Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Watu hutumia limau na Asali kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade”.
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
*Chukua asali mbichi nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa nusu lita.
Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalsini lita 2 ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5. Ihifadhi katika friji isiharibike.