Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama wanaweza kujifunza kuchukia, basi wanaweza kufundishwa kupenda, kwa sababu kwa kawaida ni asili yake upendo kuja kwa moyo wa mwanadamu kuliko kinyume chake
Ni heri kuwapenda wenzako kuliko kuwachukia kwani upendo ndio hufaidi ila si chuki.
 
Chuki hufunga akili. Inazuia ubunifu wowote wa mbinu. Viongozi hawana nafasi ya kuchukia.
Ina maana kuwa tunafaa kupendanda ili kuendelea maishani hasa viongozi. Kwa mfano; kama kiongozi wa taifa anawachukia watu katika nchi yake hatakubali kufanya kazi nao ingawa kazi hio itasaidia kuendeleza taifa lake.
 
Kabla ya kutenda jambo lolote fikiria ambavyo jambo hilo litaadhiri maisha yako
Ina maana kuwa kabla ya kutenda jambo lolote unafaa kufikiri kama ungalitendewa ungaliskia aje? Kwa mfano; kabla ya kusema mabaya kuhusu mwenzako ni vyema kufikiria ‘mtu angalisema mabaya kukuhusu ungalifurahi?’
 
Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotarajia
Ukiishi maisha yako ukifuata ndoto zako utaishi maisha ambayo utapendezwa nayo kwani mwishowe ndoto zako zitatimia ukitia bidii. Kama tujuavyo watu huangali mwisho wa safari bali si mwanzo wa safari.
 
Back
Top Bottom