Nafahamu jaribio lako ni kutaka kunikera...! ni kwel kwa sehemu nahisi kujaribika lakini nakivumilia kikero chako..!
Najua nikifika kilele cha matamanio yako ya kukeraka hata amani kidogo iliyopo itatoweka... Lakini busara ni kurejesha amani...! Kimtizamo mpaka kufikia hali hii ni dhahiri shahiri kuna mahali hapajakaa sawa... labda ni nimevuruga sheria ya mchezo ya kukomenti chochote...! lakini hainiondolei haki ya kusahihishwa kistaarabu...!
Mkuu tuheshimiane basi hata kama kinafiki kuliko kutoleana maneno yasiyofaa...! Binafsi sipendi kuona mtu ananung'unika kwa ajili yangu vivyo hivyo sipendi kumnung'unikia mtu...! Siona sbb ya kukosana na wewe kama kuna kukosoana...!
Niko simple sana na msikivu...! ni ishu tu ya kunitonya tu, Mkuu eeeh..! kuna moja mbili tatu sijapendezwa nayo... Then naomba radhi na maisha yanaendelea kwa uzuri kabisa..!!