Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kababu za yai Vinavyohitajika Nyama ya kusaga ½ kilo Mayai 5 Chenga za mikate(bread crumble) Vipande vya mikate ya French bread 3 vya kiasi Chumvi kiasi Pilipili manga ½ kijiko cha chai Pilipili nzima iliyosagwa ½ cha chai Ndimu kipande Mafuta ya kupikia Mayai 2 ya kuchomea kababu Bizari nzima iliyosagwa kijiko kimoja cha chai Kotmiri kiasi Thomu na tangawizi ya kusaga kijiko 1 cha kulia chakula Namna ya kutayarisha na kupika · Chemsha mayai mpaka yawive vizuri na uyamenye · Chemsha nyama kwa chumvi na ndimu · Ikikauka ichanganye na viungo vyote mpaka ichanganyike vizuri · Weka vipande vya mkate ambavyo unatakiwa uvivuruge kwa Kuvishikia kwa maji kidogo kidogo · Vunja yai moja na uchanganye kwenye mchangangiko wa nyama · Fanya mviringo na uweke kishimo cha kuweka yai ulolichemsha · Lifunge ndani vizuri yai kwenye nyama lisionekane · Piga yai kwenye kibakuli na uchovye mviringo na ugaragize kwenye chenga za mkate na tayari kwa kuichoma kababu ndani ya mafuta yaliyokuwa tayari yamepata moto · Ikiwiva itoe na uiweke kwenye chujio kugida mafuta na tayari kwa kuliwa Kidokezo Unaweza kufanya kababu kwa kutumia kuku au tuna na pia unapochemsha nyama, igonge gonge kwa mwiko ili ivurugige vizuri isifanye madonge na ukiwa unayo food processor ni vizuri kuichanganya humo pamoja na mikate na viungo
 
MILK SHAKE Ingredientz Maziwa ya maji....i ltr Ndizi mbivu ....mbili Red rose.....just a little Sukari .......... Chemsha maziwa yagandishee yawe barafu......yakisha kuganda kata vipande vpnde vya barafu blend pamoja na ndizi mbivu na maziwa ya maji na sukar na red rose .-.......
 
Vitumbua vya Nyama Mahitaji Nyama ya kusaga robo Kitunguu 1 Kitunguu thoum nusu kijiko Karoti 1 Pilipili hoho nusu Mayai 5-6 Baking powder nusu kijiko kidogo Pilipili manga kiasi Pilipili mbichi(ukipenda) Chumvi kiasi Namna ya kupika vitumbua vya nyama Hatua kwa hatua Safisha nyama, uitie thoum, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri kata vitunguu, hoho, pilipili na uvichanganye na mayai, kisha vyote vitie kwenye nyama yetu Weka kwenye blender mchanyanyiko wetu uusage kidogo ila usiwe laini sana. Ikiwa tayari, mimina katika bakuli. Kisha tia baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri. andaa chuma cha kukaangia vitumbua, bandika jikoni, weka mafuta kidogo. Mafuta yakipata joto chota kwa upawa mchanganyiko wetu utie kwenye kikaango, vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive kisha uvitoe. Endelea kuchoma hadi viishe vyote, hapo tunakua tumemaliza upishi wetu wa vitumbua Natumai tumeenda sambamba hatua kwa hatua jinsi ya kupika vitumbua vya nyama
 
Maini ya ng'ombe (fried) Unahitaji Maini kg 1 Kitunguu swaum kijiko 1 cha chakula Chumvi kiasi Apple cider au ndimu kijiko 1 cha chai Corriander powder nusu kijiko cha chai Pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chai Mint sauce nusu kijiko cha chai Kitunguu maji 2 ( katakata) Giligilani fresh kijiko 1 cha chai Tangawizi ya unga nusu kijiko cha chai Olive oil vijiko 3 vya chakula Njia Toa ngozi ya juu ya maini kama ipo. Katakata maini na uyaoshe mara 2 tu vzr. Kisha chukua maji yaliyochemka na umimine kwenye maini yako. Yaache kwa sekunde 5. Chuja maji vzr yabaki makavu. Tia viungo vyote na uweke kwenye friji kwa saa 1. Bandika chuma kisichoshika (non stick) na uyaweke maini kwa moto mdogo kwa dk 2 kisha ongeza moto na ukaange mpk yatakapokauka na kutoa mafuta.. nakula na chips na salad
 
*HALF MOON...* *VIPIMO* Unga wa ngano kilo 1 siagi robo Mayai 2 bt sio lazima arki vanilla Maji kwaajili yakupondea hilik..kias lainii....ukipenda sukar laini...kias..upendacho bp kijiko kimoja cha chai Njia... weka unga tia mayai...na siagi...hilik ukipenda...arki...changanya ponda na maji.. fanya madonge...sukuma km chapat...usiwe mnene sana wala mwembamba sana... kata kwa cutter yke...yenye umbo la nusu mwezi...au kwa kikombe cha kahawa... bake..km vileja na oven..vtowe vikiwa vyeupe..visipge rangi.. tia sukar vikiwa vimotomoto km doughnuts..
 
NUNGHATAI 2 (eggless ) siagi 250gms samli 200gm sukari kikombe 1 4 cups unga vanila ya unga hiliki Rangi upendanyo. Kungu manga nusu kijiko cha chai b.powder kijiko cha chai 1 method changanya samli na siagi kwa mixture mashine iwe nyeupe na laini tia sukari endelea kusaga tia vanila na b.powder sanga uzuri tia kungumanga ikisha tia unga wako chanyanya kwa Mkono ukishachanyanyika uzuri fanya viduara vidogo gandambiza kwa kidole cha gumba tia rangi bake kwa 25 minutes Usifungue oven bada dakika hizo zima jiko ziwache nunghatai kwa oven for 15 minutes than zitowe tayari kwa kuliwa
 
NUNGHATAI 2 (eggless ) siagi 250gms samli 200gm sukari kikombe 1 4 cups unga vanila ya unga hiliki Rangi upendanyo. Kungu manga nusu kijiko cha chai b.powder kijiko cha chai 1 method changanya samli na siagi kwa mixture mashine iwe nyeupe na laini tia sukari endelea kusaga tia vanila na b.powder sanga uzuri tia kungumanga ikisha tia unga wako chanyanya kwa Mkono ukishachanyanyika uzuri fanya viduara vidogo gandambiza kwa kidole cha gumba tia rangi bake kwa 25 minutes Usifungue oven bada dakika hizo zima jiko ziwache nunghatai kwa oven for 15 minutes than zitowe tayari kwa kuliwa
 
mishkaki ya prons... prons....1 kg Vitunguu maji pilipili boga thom.. tangawizi uzile Pilipilimanga chumvi ndimu..kubwa moja mama sita source vijiko viwili vya kulia olive oil kijiko cha kulia chumvi pilipili ya kuwasha.. safisha prons mkia usiutoe ...weka spices zote ...wacha kama saa ili viungo vikolee... kata Vitunguu maji vipande vipande pamoja na Pilipili boga... chukua vijiti vya mishkaki anza kupanga prons kitunguu prons pilipili size unayotaka ... chukua tray weka jikoni ipake mafuta kidogo ...panga mishkaki yako kwenye trey kila mara uwe unageuza mpaka wawive..
 
Cake ya zabibu na nazi Cup 1 sukari Cup 1 mafuta Cup 1 na nusu unga Mayai 5 Ts 2 maziwa ya unga Nusu cup nazi kavu Vinegar ts 1 Maganda ya machungwa grate kdg Bp ts 1 Bicabonat ts 1 Maji nusu cup Zabibu kavu kdg Piga mafuta na sukari kisha tia mayai na vanila Baadae tia vitu vyote weka unga wako kwenye trey ya cake tupia zabibu juu choma
 
*CURRY PRAWNS* *MAHITAJI* Prawns kama nusu kilo (walio safishwa) Kitunguu 1 size ya kati (chopped ) Nyanya 2 kubwa (tomatoes chopped) Kitunguu saum (garlic) 1 tsp Tangawizi 1tsp Tui la nazi kikombe kasorobo 3/4 Bizari 1 tsp Curry powder (simba mbili) 2 tsp Pilipili ya unga 1 tsp Limau au ndim kipande Chumvi kiasi Mafuta ya kupikia 2 tblsp Tsp = kijiko kidogo cha chai Tblsp= kijiko cha kulia *MATAYARISHO* Weka mafuta kwenye frying pan iliyo na shimo au dish. Kaanga vitunguu kwa dakika 2 mpaka viwe laini visiwe vyekundu. Weka tangawizi, garlic, bizari na curry powder changanya kwa nusu dakika weka tomatoes. Wacha tomatoes ziive vizuri halafu weka pilipili ya unga na chumvi. Mix kwa dakika 1 weka tui la nazi acha lichemke lakini koroga usiachie mkono ili lisikatike. Kama dakika 3 halafu weka prawns kwenye tui wacha waive. Hawachukui muda kuiva. Wakisha kuiva weka ndimu onja kama kila kitu kiko sawa. Tayari kwa kuliwa na wali ama ugali au unachopenda. ENJOY.
 
PANDAN CHIFFON CAKE VIPIMO MAHITAJI: A Majani ya Pandan 20 Tui la nazi 80-90ml Viini vya mayai 6 Sukari 25g Mafuta 70ml Unga Kikombe 100g MAHITAJI: B Ute wa yai 7 Sukari 100g Unga wa sembe 12g NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 1. Kata majani ya Pandan kisha blend na tui la nazi hadi yawe laini, kisha chuja na upime Pandan Juice. 2. Chukua Viini vya mayai na sukari changanya koroga kwa pamoja hadi kuchanganyika. 3. Mimina Mafuta na Pandan Juice kwenye mchanyanyoko na endelea koronga. Kisha weka unga na uendelee kukoroga akikisha usiwe na madoge. 4. Washa jiko lako (Oven) kwa moto 325°F / 160°C 5. Saga ute wa yai kwa dakika chache kwa kutumia mashine ya kukorogea cake (cake mixer) mpaka povu kujaa. Tia unga wa sembe na sukari blend mpaka Cream ijae juu. 6. Tia kwa pamoja mchanganyiko wa Viini vya Mayai na wa Ute wa yai. Koroga mpaka uchanganyike kuwa rangi moja. 7. Pakaza Siagi kwenye sifuria ya kuchome cake na Mimina Unga, Sawazisha ukae sawa. 8. Ingiza sifuria ndani ya jiko (oven) kwa dakika 50 hadi 55 Keisha toa. 9. Wacha cake ipoe kisha tumia kisu kuachanisha sifuria na cake kutoka ndani ya sifuria na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Enjoy!
 
Toffee Cake Mayai 4 Cup 1 sukari na vanilla piga dakika 3 halafu tia mafuta nusu cup na maziwa mtindi cup 1 mix uzuri mwisho tia unga cups 2 na ts 1 bp na ts 1 hiliki mix uchome Ikipoa mwagia toffe Yayusha sukari cup 1 siagi tb 1 na nestle cream ukipenda mwagia nuts na nazi kavu juu -
 
Toffee Cake Mayai 4 Cup 1 sukari na vanilla piga dakika 3 halafu tia mafuta nusu cup na maziwa mtindi cup 1 mix uzuri mwisho tia unga cups 2 na ts 1 bp na ts 1 hiliki mix uchome Ikipoa mwagia toffe Yayusha sukari cup 1 siagi tb 1 na nestle cream ukipenda mwagia nuts na nazi kavu juu -
 
FLOWER RICE* (Wali wa maua) "Riceps" Vitu vinavyohitajika. 1)mchele kilo 1 2)njegere glass moja ndogo 3)nyanya 1 4)vitunguu maji viwili 5)Nazi 1 6)Carrot 2 7)pilipili oho 1 8)chumvi kiasi chako JINSI YA KUPIKA Chukuwa mchele wako kisha uoshe vizuuri kwa maji safi,kisha chukuwa njegere zako zichanvue na uzioshe kisha zichemshe hadi ziive ,kisha katakata vitunguu silece na vikaange mpaka viwe brown(kahawia) kisha kata kata carrot na p.oho silece zikaange pamoja na vitunguu vyako ,kisha weka nyanya ,nyanya unaikwangua au unaisaga baada ya hapo tia njegere zako umo umo kwenye nyanya ,oho,vitunguu na carrot ,kisha chukua mchele wako weka umo umo kisha tia weka maji ya moto kiasi tia na tui LA Nazi acha uchemke mpaka ukauke na ugeuze na wali wako utakua tayari kwa kuliwa.waweza kuhula kwa mboga yoyote ile
 
BORESHA MLO WAKO KWA KUTUMIA SALAD!! SALAD YA MAYAI YA KUCHEMSHA Mahitaji: Kabichi au letus Mayai yaliochemshwa 3 na kutolewa maganda Karot kubwa 1 Kitunguu kikubwa 1 Majani ya kotmir kiasi Maji ya ndimu au vinegar kijiko 1 Chumvi ukipenda JINSI YA KUANDAA. 1.Osha mahitaji yote vizuri kasoro mayai,chumvi na n maji ya ndimu 2.Katakata mahiataji ktk shepu upendayo,kisha pangilia vizuri kwa mtindo unaokupendezea juu weka vipande vya mayai 3.Nyunyizia maji ya ndimu au vinegar kisha nyunyizia chumvi ukipenda.Waweza kula na chakula chochote upendacho,huzisha hamu ya kula pia.ENJOY!! NB: Mayai waweza kata slice au vyovyote upendavyo
 
WALI WA MANJANO Mchele kilo 1 (wa basmat au kawaida) Binzari manjano kijiko 1 Chumvi kiasi chako Vitunguu maji vikatekate 2 Kitunguu saumu kilichopondwa kijiko 1 Mafuta kiasi Maji kiasi Karoti zilizo katwakatwa vipande 2 Njegere ziwe zimegandishwa kutoka ktk fridge kikombe 1 JINSI YA KUPIKA: 1.Kaanga vitunguu kwa mafuta mpaka vibadilike rangi kisha weka kitunguu swaum,kisha binzari ya manjano kaanga kidogo 2.Tia maji yaache, yakichemka tia mchele, njegere ,karoti na chumvi, na uongeze mafuta kidogo,kisha wacha wali uchemke kama wali wa kawaida 3.Ukishakaukia weka moto wa juu au kwenye oven kwa moto wa 250 c baada ya dakika 20 wali utakua tayari.waweza kula na mchuzi wowote au mboga.ENJOY -
 
Visheti vya tende na maziwa Tende iliyosongwa Siagi nusu Mafuta glas1 Maziwa glas1 Arki Bp kijiko1 Unga kilo na robo Sukari iliyosagwa Namna ya kuandaa Changanya siagi na mafuta saga tia maziwa arki na bp saga tia unga kilo changanya tia na ule robo changanya vizuri ikisha chukua saiz chawanya kwenye kibao tia tends kati usokote na utate Fanya ivyo mpaka umalize na ukiona vinakunata shikilia unga,tia kwenye oven weka moto wa chini tuu havitakiwi kupiga ranging juu,vikiwa tayari vitie sukari ya unga au icng -
 
KASHATA ZA MAZIWA(FUDGE) Siagi 1/2 kikombe Sukari kikombe 1 Maziwa mazito (condensed milk) kikopo 1 Maziwa ya maji 1/2 kikombe Vanilla kijiko 1 JINSI YA KUPIKA 1.Weka sufuria jikoni ikipata moto weka siagi kisha tia sukari koroga tia vanilla ,maziwa ya maji na maziwa mazito kisha koroga kwa dakika 10 usiachie mpaka siagi iyeyuke vizuri kisha epua 2.Paka tray au sinia mafuta kisha mimina mchanganyiko wako,uache kwa dakika 10 kisha weka katika fridge kwa masaa 6 itoe itakua tayari imeganda vizuri katakata vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa.Ni tamuuuu!!! ENJOY!!! NB: Waweza kuongeza chocolate ukipenda kwa kuikata vipande vipande na kutia katika mchanganyiko wako wakati ushaepua ili chocolate isiyeyuke.
 
KASHATA ZA MAZIWA(FUDGE) Siagi 1/2 kikombe Sukari kikombe 1 Maziwa mazito (condensed milk) kikopo 1 Maziwa ya maji 1/2 kikombe Vanilla kijiko 1 JINSI YA KUPIKA 1.Weka sufuria jikoni ikipata moto weka siagi kisha tia sukari koroga tia vanilla ,maziwa ya maji na maziwa mazito kisha koroga kwa dakika 10 usiachie mpaka siagi iyeyuke vizuri kisha epua 2.Paka tray au sinia mafuta kisha mimina mchanganyiko wako,uache kwa dakika 10 kisha weka katika fridge kwa masaa 6 itoe itakua tayari imeganda vizuri katakata vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa.Ni tamuuuu!!! ENJOY!!! NB: Waweza kuongeza chocolate ukipenda kwa kuikata vipande vipande na kutia katika mchanganyiko wako wakati ushaepua ili chocolate isiyeyuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…