Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ROSTI LA CHAZA NA NYANYA CHUNGU MAHITAJI Chaza Nyanya chungu Tungule Kitunguu maji Kitunguu thom Karot Pilipili boga Pilipili refu za kuwasha Tangawizi kdg ukipenda Bizari kdg ukipenda Nazi Safisha vizuri chaza zko zisiwe na Michanga zichemshe kdg Katia vitu vyako tungule, vitunguu, keroti, pilipili boga, na vyengnevyo wacha vichemke kdg menya Nyanya zko zipasue kdg kati Tia Nyanya mimina tui lako kiasi la mwanzo weka mwisho funika kdg ziive vzr karibu ya kukauka Tia tui lako la mwanzo ikiwa Tayari ipua Huliwa kwa wali au mikate au upendacho Yummy
 
VITUMBUA VYA MAYAI KATIKATI Mahitaji: mchele vikombe 2 1¾ vikombe tui la nazi (vugu vugu) Hamira pakiti 1 (70 grams) ½ - 1 kikombe cha sukari UKIPENDA KUONGEZA : Unga wa posho AU unga wa ngano vijiko 1-2 Mafuta ya kupikia Mayai 10. MATAYARISHI. 1. Roamisha mchele usiku kucha. 2.Saga mchele na hamira, tui la nazi,sukari pamoja na unga wa ngano au wa posho kama utatumia. 3.Funika uweke kando unga uumuke. 4.Chemsha mayai mpaka yaive, yatoe maganda, kisha uyakate pande mbili. Weka kando. UPISHI; ANGAZO: Unapika kama unavyopika vitumbua vya kawaida, tofauti ndogo tu ni hiyo kuongeza yai kati! 1. Baada ya kutia unga kwenye chuma, unaongeza na nusu yai katikati. Wacha unga uwive kidogo kisha geuza na uendelee kupika kama kawaida. -
 
YAI NA UNGA WA DENGU MAHITAJI Mayai 3 Unga Wa dengu 1/4 Giligikiani kidogo (kama ukipenda) Tangawizi 1/2 kijik cha chain Kitunguu maji 2 Chumvi kiasi chako Hoho nusu Maji kikombe 1 JINSI YA KUANDAA Weka unga Wa dengu ktk bakuli tia maji na chumvi weka pembeni. Katakata kitunguu, giliguliani, hoho, na usage tangawizi na weka pembeni. Chukua mayai yagonge na mimina ktk unga koroga kuchanganya, kisha weka viungo ulivyo katakata kisha changanya kwa pamoja. Weka kikaango jikoni tia mafuta kiduchu ya kichemka chota mchanganyiko wako kwa kutumia upawa, mimina kwa Staili ya chapati ikiiva geuza upande Wa pili kisha toa na hapo itakuwa tayari kwa kuliwa.
 
*Vitumbua vya unga wa Mchele na ndizi mbivu,* Mahitaji:- Unga wa mchele vikombe 2 Hamira kijiko 1 chakula Ndizi mbivu 1, ilopondwa Sukari 1/4 kikombe Tui la nazi zito vugu vugu kikombe1 1/2 Maji 1/2 kikombe Nazi ilokunwa 2 kijiko cha chakula ( hapa nimetumia Nazi kavu) Iliki kijiko 1 cha chai Ute wa yai 1 MATAYARISHO NA NAMNA YA KUPIKA: 1. Tia mahitaji yote katika bakuli isipokuwa ute wa yai , kisha koroga vizuri kuchanganya hadi upate unga mlaini usiwe na mabonge. 2. Funikia kisha acha uumuke kwa muda wa dk 30 au zaidi hadi ujae mara mbili. Tia ute wa yai kisha changanya vizuri 3. Tia chuma cha vitumbua jikoni juu ya moto wa kiasi, choma vitumbua vyako Kama kawaida hadi vipate rangi pande zote mbili. Enjoy! -
 
FB_IMG_1506836492571.jpg
 
Back
Top Bottom