VITUMBUA VYA MAYAI KATIKATI Mahitaji: mchele vikombe 2 1¾ vikombe tui la nazi (vugu vugu) Hamira pakiti 1 (70 grams) ½ - 1 kikombe cha sukari UKIPENDA KUONGEZA : Unga wa posho AU unga wa ngano vijiko 1-2 Mafuta ya kupikia Mayai 10. MATAYARISHI. 1. Roamisha mchele usiku kucha. 2.Saga mchele na hamira, tui la nazi,sukari pamoja na unga wa ngano au wa posho kama utatumia. 3.Funika uweke kando unga uumuke. 4.Chemsha mayai mpaka yaive, yatoe maganda, kisha uyakate pande mbili. Weka kando. UPISHI; ANGAZO: Unapika kama unavyopika vitumbua vya kawaida, tofauti ndogo tu ni hiyo kuongeza yai kati! 1. Baada ya kutia unga kwenye chuma, unaongeza na nusu yai katikati. Wacha unga uwive kidogo kisha geuza na uendelee kupika kama kawaida. -