Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndiyo uzuri wetu huo kama binadamu. Kila mmoja wetu ni tofauti na mwenzake. Na katika utofauti huu ndimo kuna upekee na uthamani wetu. Tunakamilishana, tunategemeana - katika uhasi na uchanya wetu. Na kila mmoja wetu ana uzuri wake - hata awe mwovu namna gani (and vice versa). Cha muhimu ni kuvumiliana. Ndiyo maisha. Ndivyo tulivyoumbwa !!!

[emoji117][emoji117][emoji117] Tabia yako ya uwazi na kupambana nilishaiona tangu zamani. You never back off. Mtanange ule uliokupigisha ban humu ulithibitisha hilo. Nakuitaga mwanamke wa shoka. Na watu wengi huwa hawategemei ungangari wa aina hii kutoka kwa mwanamke. Pengine ndiyo sababu inayofanya wengine mpaka wadodose hata jinsia yako wakidhani kuwa eti u kavulana. Numbisa !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…