5. Suala la Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao wana uhitaji tofauti.
Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.
Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.
6. Vipaumbele katika Maisha
Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.
Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.
7. Uaminifu
Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.
Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu lakini huchukua muda mrefu sana.

Suala linalofanana na hili ni uhusiano na baadhi ya marafiki wa jinsia moja ambao wanachukuliwa kuwa mfano mbaya na mpenzi wako. Kama haiwezekani kutowasiliana na kuonana na wapenzi wa zamani au marafiki, basi ni vyema wakawa marafiki wa familia nzima na mawasiliano yoyote kati yenu nao yawe wazi pasipo kificho.
8. Wapenzi,Marafiki na Maisha ya Zamani
Mojawapo ya vyanzo vya ugomvi kati ya wapenzi ni wapenzi wa zamani. Mawasiliano ya aina yoyote na wapenzi wa zamani huleta wasiwasi mkubwa kwa mpenzi wa sasa. Ni kitu ambacho wapenzi wawili wanahitaji kuongea na kupanga jinsi ya kuepukana na matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na historia zao za maisha.
Kuepukana na hii ni vyema kuvunya uhusiano wa aina yoyote na wapenzi wa zamani labda tu kama wapenzi hao ni wazazi wenza au mnafanya kazi pamoja na ni ngumu kutokuonana au kuwasiliana.

9. Watoto
Suala la uleaji na ukuzaji wa watoto linasababisha ugomvi mara nyingi kati ya wazazi. Jinsi gani mtoto avae au shule ipi aende linapelekea wazazi wengi kugombana.
Ni jambo la muhimu sana kukubaliana juu ya mambo ya msingi juu ya malezi ya watoto. Tofauti za wazazi ziangaliwe kwanza vinginevyo zitaingilia malezi ya watoto na kusababisha ugomvi juu yao.

10. Kazi za Nyumbani
Imekuwa kama utamaduni kwa waafrika kuacha kazi nyingi kama si zote za nyumbani kwa mke. Kwa Wanawake ambao wanafanya kazi pia inakuwa ngumu sana. Hili linasababisha pia ugomvi kwa wapenzi nyumbani. Kama nguo ambazo mume anazivaa na kuzichafua tu bila ya kujali kuwa mweza wake ataumia wakati wa usafi na ikiwa yeye mwenyewe hajishughulishi na kufanya baadhi ya kazi za nyumbani ni wazi itasababisha ugomvi.
Ni vyema wanaume kuchukua baadhi ya majukumu nyumbani hata kama kutengeneza bustani au kulisha chakula mifugo.
Faida ya Ugomvi kati ya Mke na Mme Katika Mahusiano
Japokuwa ugomvi ni kitu cha kuepuka,lakini kina uzuri wake katika mahusiaono kama kikichukuliwa vizuri na kutumika kama kioo.
Kama mtu anagombana na mpenzi wake kwa madhumuni ya kuboresha ni kitu kizuri. Hii inaonesha kuwa anahitaji kuwa na wewe na anahitaji amani.
Ugomvi na mifarakano pia inatoa nafasi kwako kujiangalia vizuri na kama kinacholalamikiwa na mwenzio kina ukweli basi ni nafasi ya kujirekebisha.
Ni mategemeo kuwa kuna kipindi ambapo ugomvi utakuwa mkubwa na baadae wapenzi hao wataelewana na kurekebisha mambo yao.
i. Ugomvi Unatoa Nafasi ya Kuongea Mambo Magumu
Wakati mwingine mazungumzo ya kawaida hayatoi nafasi ya wapenzi wawili kusema yale ya ndani na yanayozizonga nafsi zao. Ugomvi hufungua milango ya hisia za ndani na huenda vyanzo vya matatizo vikawekwa wazi na hivyo kufanyiwa kazi.
ii. Ugomvi unaonyesha Kuwa Mnajali na Mnataka Maboresho
Katika uhusiano ambao wenza hawajali,au hawana malengo ya muda mrefu huwa hawatoi duku zao juu ya utofauti na wapenzi wao.Hivyo wapenzi wanaogombana wanaonesha kuwa wana nia ya dhati na mwenzao na sio tu kupitisha muda.
Kwa muwa ugomvi unaibua hisia zilizojificha toka kwa wapenzi,ni wakati mzuri kuona matatizo ya kila mmoja. Na kama wapenzi hao wana nia ya dhati ya kuwa pamoja basi watafanyia kazi tofauti na mataizo waliyonayo. Hivyo kuboresha mahusiano yao
Kuna sababu nyingine nyingi ambazo zinachangia ugomvi kati ya mke na mme katika mahusiano lakini haya ni yale yanayotokea katika mahusiano mengi.
Imeripotiwa kuwa Bayern Munich wamepata meneja mpya na bosi wa zamani wa klabu hiyo Pep Guardiola alishiriki kuwashauri katika uteuzi huo.
Mabingwa hao wa Ujerumani walimtupia virago Carlo Ancelotti wiki iliyopita kufuatia kichapo cha 3-0 dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa.
Kocha msaidizi Willy Sagnol amechukua mikoba kama kama kocha wa muda, na Bayern ilipata sare ya 2-2 Jumapili katika mechi ya kwanza kwa Mfaransa huyo.
Alexandre Lacazette amebainisha kuwa uwepo wa Alexis Sanchez kwenye timu ya Arsenal ulimshawishi kujiunga na klabu hiyo, wakati mshambuliaji huyo anashinikiza kuondoka.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa amekuwa usajili wa rekodi kwa Gunners majira ya joto baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 46.
Lacazette amedai kuwa alishawishika kutua Emirates kutokana na wachezaji bora waliomo klabuni humo, akiamini kwamba Sanchez ni mchezaji muhimu licha ya nyota huyo kutaka kuondoka.
Inafahamika kuwa Gerard Pique alikuwa katika hali ya kukata tamaa alipokutana na waandishi wa habari baada ya Barcelona kucheza dhidi ya Las Palmas kwenye uwanja usio na mashabiki Camp Nou Jumamosi.
Yeye na wachezaji wenzake walilazimishwa na Ligi ya Soka (LFP) kucheza mechi wakati watu wao waliokuwa wakitaka kupiga kura ya uhuru wa Katalunya wakishambuliwa kikatili na polisi waliotumwa na serikali ya Hispania kuzuia kura ya maoni ambayo ilidaiwa si halali kisheria.
Imekuwa siku ngumu sana, huenda ni siku mbaya zaidi tangu nianze kucheza soka la kulipwa," beki huyo alisema huku machozi yakimbubujika. "Lakini maoni yangu yatakuwa na tija kidogo tu."
Ingawa Pique hakuwa sahihi katika maneno yake. Maoni yake yana tija, kwa watu wengi; kwa wale wenye imani sawa na yeye kwamba watu wa Katalunya wanastahili kupewa haki ya kuamua kubaki sehemu ya Hispania au la!
Kwa hakika, Pique alipomponda waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy, ilikuwa habari maarufu.
"Yeye ni rais wa serikali, ambaye huzunguka ulimwenguni, na hajui kuongea Kiingereza," Mkatalani huyo alibwata. "Huo ndio upeo wake."