Waziri wa michezo wa Catalonia, Gerard Figueras, amedai kuwa Barca inaweza kucheza Ligi Kuu Uingereza ikiwa mkoa huo utafanikiwa kujitoa Hispania, akiitaja Swansea City kama mfano wa klabu kutoka nchi tofauti inayocheza Ligi Kuu Uingereza.
"Ikiwa uhuru utapatikana, timu za Catalan zinazoshiriki La Liga - Barcelona, Espanyol na Girona - zitaamua wapi zinataka kucheza: Aidha kwenye Ligi ya Hispania au nchi za jirani, kama Italia, Ufaransa au Ligi Kuu Uingereza," alisema Figueras.
"Sasa katika Hispania kuna timu tatu kutoka nchi nyingine ambazo zinacheza ligi ya taifa: Klabu kutoka Andorra kwenye soka na mpira wa kikapu.
"Monaco inacheza Ufaransa, Uingereza zipo klabu za Wales. Sidhani kama Uefa wana sababu yoyote kuizuia klabu kucheza ligi tofauti na nchi yake."
Barcelona wamekuwa mabingwa wa La Liga mara 24, lakini wamezidiwa na mahasimu wao wakubwa Real Madrid (33).