Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kila mtu anahitaji kupendwa kama mtu,mzazi,mwenza,mtoto au mfanyakazi. Inaleta raha na faraja kubwa moyoni. Lakini wakati mwingine si rahisi sana kupendwa na watu wengi. Wengine wanasema kuwa haiwezekani kupendwa na kila mtu,kwasababu kila mmoja ana vigezo tofauti vya kuchagua nani anampende na kinyume chake
 
Ila kuna vigezo ambavyo watu wengi wanathiriwa navyo juu ya maamuzi yao ya kupenda. Kwakweli maamuzi haya si ya hiyari ila yanakuja kwa hisia zaidi kutoka katika mawazo ya kina ambayo yanaongoza hisia za watu.

Hisia hizi zinajijenga taratibu ndani ya moyo wa mtu kutokana na matukio yanayotokea kila siku au kila mara na kuwekwa katika mawazo ya kina.
 
Ili upendwe na watu unatakiwa kujenga tabia amabazo watu watazipenda na hivyo wewe mwenyewe kupendwa. Kumbuka unatakiwa kujenga tabia na si kufanya kama roboti. Haya yanatakiwa kutoka ndani ya moyo wako. Unatakiwa kuwa halisi na sio kuigiza vinginevyo hutapata matokeo mazuri.
 
Tabia 8 Kuu za Kupendwa na Watu
Kuna mambo mengi ambayo yanachangia kupendwa lakini haya ni yale ambayo nimeyaona yanamchango mkubwa na kama yakifanywa kwa ukamilifu yataweza kukupa matokeo mazuri na ukafanikiwa sana katika kuishi na kufanya kazi na watu sehemu yoyote iwe ni kazini nyumbani au sehemu nyingine za kijamii.
 
Gusa nyoyo zao-Shiriki Hisia zao

Binadamu wanaongozwa na hisia zaidi,maamuzi mengi bado yanategemea hisia kuliko utashi.

Ingia katika nyoyo zao na ufahamu nini kimo ndani na uwe mshiriki.

Fahamu kuhusu afya zao kwa kwenda zaidi ya salamu ya kawaida. Uliza juu ya watu wanaowapenda sana na wanaomaanisha maisha yao kama watoto,wenza au wazazi.
 
Uliza maswali kama “Watoto wanaendeleaje? Wako darasa la ngapi?” ukiweza taja majina yao katika mazungumzo “John na Maria wanaendeleaje? Wameanza shule?”

Kama ni kazini ulizia kuhusu mradi wa mfanyakazi mwenza wako, “Umefikia wapi na mradi wako wa kutokomeza malaria?”

Shiriki katika mambo ya kijamii,sikukuu za kuzaliwa,misiba na sherehe kama harusi.
 
Kuwa Msikivu

Katika mazungumzo,jenga tabia ya kusikiliza zaidi kuliko kuongea. Ongea pale mwingine anapokuwa amemaliza kusema. Usifanye kitu chochote kingine ukiwa unaongea na mtu kama vile kutuma ujumbe katika simu na muangalie usoni. Kwa namna hii unaonesha kujali anachosema na hukupandisha katika alama za kupendwa.
 
Kama uko katika nafasi za uongozi iwe nyumbani,kazini au sehemu nyingine,toa nafasi kwa watu kuongea na kutoa mawazo na hisia zao,kisha toa mtazamo wako au ushauri juu ya suala husika. Wakati unafanya hivyo usioneshe hata kidogo kuwa mawazo yao hayana maana. Sababu kila jambo lina maana,kama simkwako basi kwa aliyeliongea. Jali mawazo ya kila mtu
 
Kuwa Mkweli na Timiza Ahadi

Sema kweli mara zote,ukweli utalkuweka huru lakini kubwa zaidi watu watakupenda na watakuwa wakweli kwako pia.

Ahidi kilichopo ndani ya uwezo wako na utimize kwa wakati uliosema kuwa utafanya.
 
Onesha Mfano,Tembea Katika Maneno Yako

Ongoza kwa mfano,fanya yale unayoamini na unayoyasema. Katika nafasi za uongozi ni vizuri kufanya japo kwa kiasi fulani kile unachowapangia wengine kufanya. Katika mazingira ya nyumbani unaweza ukaamua kulisha mifugo wikiendi mojaau kukata majani viungani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…