Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

na ulemavu wa vidole. Pia uweza kusababisha ugonjwa wa arthritisi kadiri umri unavyoongezeka na matatizo ya uzazi katika nyonga kutokana na kuelemewa na uzito asa kwenye jointi za magoti na nyonga.

ILI KUEPUKA MADHARA HAYA ZINGATIA YAFUATAYO
Fanya mazoezi ya kunyoosha miguu kabla ya kuvaa viatu hivi
Vaa viatu virefu kiasi maana kila urefu kwani madhara yake uongezeka kutokana na urefu wa viatu
 
Nunua viatu hivi wakati wa mchana mguu wako unakuwa umetanuka kidogo hivyo utaweza kupata size inayokufaa.
Usivae viatu virefu vilivyochongoka upande wa kidole gumba tu
Vaa viatu vyenye ngozi kwa ndani ili kuwezesha miguu kukaa vizuri.
Kuwa na pea nyingi za viatu ili kukuwezesha kubadilisha inapotokea madhara
Usivae sana wakati unatembea mwendo mrefu, wa haraka, na unatumia usafiri wa uma.
 
UNAWEZA KUSHUSHA PRESHA KWA KUFANYA HAYA

Mitindo ya maaisha tunayoishi na vyakula tunavyokula hutuweka katika hatari ya kusumbuliwa na shinikizo la damu(Presha). Hii hutokea pale presha inapoongezeka zaidi ya 120/80. Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kupunguza presha na hivyo kuepuke hatari ya kupata shambulio la moyo, kiharusi na figo kushindwa kufanya kazi.
 
Punguza kiasi cha chumvi, hii itakusaidia kushusha presha na hivyo kuepuka matumizi ya dawa. kumbuka sio tu chumvi ya kuweka kwenye chakula bali hata vyakula vinavyouzwa vimeandaliwa tayari huweza kuwa na chumvi kiwango kisichostahili. unaweza kutumia viungo tofauti vya kuongeza ladha ya chakula kama chili, limao, na tangawizi.
 
Screenshot_2017-10-04-22-22-54.png
 
Back
Top Bottom