Punguza kiasi cha chumvi, hii itakusaidia kushusha presha na hivyo kuepuka matumizi ya dawa. kumbuka sio tu chumvi ya kuweka kwenye chakula bali hata vyakula vinavyouzwa vimeandaliwa tayari huweza kuwa na chumvi kiwango kisichostahili. unaweza kutumia viungo tofauti vya kuongeza ladha ya chakula kama chili, limao, na tangawizi.