Sio kongosho peke yake ndio inatengeneza vimeng’enya chakula ndani ya mwili bali vimeng’enya chakula hivi hutengeneza huweza kutengenezwa sehemu nyingine ndani ya tumbo ili kufanya kazi ya umeng’enyaji kwa ufani
Homoni hizi baada ya kuzalishwa ndani ya kongosho husafirishwa na damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hizi ni tofauti na vimeng’enya chakula ambavyo huingia moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba kupitia mrija wa kongosho.
Homoni ya insulini hii kazi ya kubwa mwilini ni kupunguza kiwango cha sukari damu. Sukari huweza kuongezeka kwenye damu kwa mtu kua na aina ya lishe yenye sukari nyingi.
Endapo sukari itakua imeongezeka kwa wingi kupita kiwango cha kawaida kwenye damu, Kongosho uanza kuzalisha homoni ya insulini ambayo hufanya kazi ya kubadili kiwango cha glukosi kilichozidi kwenye damu na kuifanya kuwa glaikojeni ambayo huenda kuifaziwa sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye misuli na kwenye ini. Hivyo basi hupunguza kiwango cha glukosi kwenye damu.
Homoni hii ya glukagoni hufanya kazi ya kubadili sukari iliyotunzwa (glaikojeni) kwenye ini na misuli kuifanya kuwa glukosi ya kawaida ambayo huingizwa kwenye damu na kufanya kiwango cha glukosi kwenye damu kurejea katika kiwango chake cha kawaida.
Pia tutambue kwamba kushindwa kwa kongonsho kuzalisha ipasavyo homoni ya insulini ndio sababu kuu ya kiwango cha sukari kupanda kwenye damu na kusababisha ugonjwa wa kisukari.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.