Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni jambo lisilo shaka kuwa iwapo kila mmoja wetu atazingatia kanuni za ulaji na unywaji sahihi, bila shaka matatizo ya moyo na shinikizo la damu yanaweza kupungua kwa kiwango kikubwa, kama siyo kutoweka kabisa.
 
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni njia mojawapo ya mafanikio makubwa kabisa ya kufanikisha na kuhakikisha afya ya mtoto anaishi vyema.

Kama kila mtoto alienyonyweshwa maziwa ya mama kwa ndani ya saa moja toka azaliwe,
upewaji pekee maziwa ya mama kwa miezi ya sita ya kwanza katika uhai wa mtoto, na kuendelea kumnyonyesha hadi umri wa miaka miwili,
 
karibu watoto 800 000 itawasaidia kuokoa maisha yao kila mwaka. duniani, chini ya asilimia 40 ya watoto wachanga chini ya umri wa miezi sita hawapewi maziwa ya mama.

Ushauri na nasaha wa kutosha kuhusu kunyonyesha na huduma ni vitu muhimu kwa ajili ya akina mama na familia katika kuanzisha na kudumisha zoezi hili la kunyonyesha.
 
Shirika la afya ulimwenguni lipo kikamilifu katika kukuza hali ya unyonyeshaji kama chanzo bora cha chakula kwa ajili ya watoto wachanga na watoto wadogo.

katika makala hii nitaonyesha ukweli unaohusu faida nyingi za kufanya, na kutoa msaada sahihi jinsi akina mama wanavyoweza kuongeza kasi ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani kote.
 
Screenshot_2017-10-06-23-34-12.png
 
Shirika la afya ulimwenguni (WHO) linapendekeza :
WHO inapendekeza kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto. Katika miezi sita, vyakula, kama vile matunda kama parachichi, ndizi na mboga, lazima aanze kuwekewa ili kumsaidia katika kipindi anachokuwa akinyonya kwa muda wa miaka miwili au zaidi.
Aidha:

kunyonyesha unapaswa kuanza ndani ya saa moja baada ya kujifungua.
kunyonyesha lazima kuwe"kwenye mahitaji", kama mara kwa mara kama mtoto anavyohitaji iwe mchana ama usiku; na
unyonyeshaji wa chupa hauna budi ziepukwe.
 
FAIDA ZA AFYA KWA WATOTO WACHANGA
Maziwa ya mama ni chakula bora kwa watoto wachanga na watoto wakuao. pia huwapa watoto wachanga virutubisho wote wanahitaji kwa ajili ya maendeleo ya afya zao.
Maziwa haya ni salama na yana kinga ambayo husaidia kuwalinda watoto wachanga dhidi ya magonjwa ya kawaida katika utoto kama vile kuhara na pneumonia, Ambavyo ndio Sababu kuu mbili za msingi za vifo vya watoto wachanga duniani kote.
 
Maziwa ya mama hupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu (bure), ambayo husaidia kuhakikisha kwamba watoto wachanga kupata lishe ya kutosha.

FAIDA KWA AKINA MAMA
Kunyonyesha pia kuna faida kwa mama. kunyonyesha maziwa ya mama inahusishwa na njia ya asili kama njia ya uzazi wa mpango (asilimia 98 huwasaidia katika katika miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa katika kuzuia mimba).
 
Pia inapunguza hatari ya kupata saratani ya matiti na ovaria baadaye katika maisha, husaidia wanawake kurudi katika maumbile yao kama kabla ya ujauzito, na husaidia kupunguza viwango vya unene uliopitiliza.

Faida za muda mrefu kwa ajili ya watoto
Kwa zaidi kuna manufaa ya kwa ajili ya watoto, kwa kunyonyesha maziwa ya mama inachangia kuwa na maisha yenye afya njema.

Vijana na watu wazima ambao walikuwa wananyonya maziwa ya mama walipokuwa watoto wana uwezekano mdogo sana wa kuwa na tatizo la unene na uzito uliopitiliza.
Pia huwa wako katika hali nzuri ya kutokupata uwezekano wa kuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari na vile vile katika kipimo cha akili huwa wako vizuri.
 
Back
Top Bottom