Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yahoo walikuwa watangulizi wa mambo mengi. Inasikitisha kuona kuwa leo ni kampuni isiyokuwa na mbele wala nyuma. Kwenye biashara bwana ukishindwa tu kuzisoma alama za nyakati na kujibadilisha kushabihiana nazo basi umekwisha !!!
 
Eti ni kweli?
Hizi ndio nchi kumi zenye wanawake wanaovutia zaidi duniani:
  1. Brazil
  2. Ukrain
  3. Urusi
  4. Uturuki
  5. Venezuela
  6. Italia
  7. Uholanzi
  8. USA / Canada
  9. Uingereza
  10. Philippines
Uwongo! Mbona Tanzania haimo?

Ni hivi: Vigezo wanavyotumia ni tofauti na vyetu. Kumbuka dhana ya uzuri hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine japo sote tunalazimishwa kuamini kuwa mwanamke mzuri ni lazima awe kimbaumbau na asiye na msambwanda. Uwongo mtupu !!!

Note: Kwa Wabrazili nakubali. Mulatto wale ngozi yao ile na miili yao ni mchanganyiko wa kushangaza....
 
Usiamini kila kitaarifu popu (Pop notification)

Mara nyingi umewahi kuona kitaarifu popu kikitokea unapotembelea tovuti fulani. Vitaarifu hivi hukutaka kusasisha ama kuweka flash player au kikikuambia kuna virusi kwenye kifaa chako. Katu usiviamini hivi kwani mara nyingi hutumika kudanganya watu ili waingize program fulani kwenye vifaa vyao ambazo zinaweza kuwa chanzo cha virusi au kudukulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…