Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ameacha mgogoro wa kikatiba!! Tume haijui ichukue hatua gani........
 
Mbali na hewa, yapo mambo kadhaa yanayochangia kupata kwikwi, ambayo ni pamoja na; kula chakula haraka haraka na hasa kama ni kikavu, kucheka sana na kwa muda mrefu, kula vyakula vyenye viungo vikali hasa pilipili kali kama hukuizoea.
 
Kumeza vitu vya moto sana na kunywa pombe kupita kiasi. Sababu hizi zinaweza kuchangia hewa kuingia kwa ghafla kwenye mapafu na kusababisha kisanduku cha sauti kufunga.
 
Sababu nyingine za ugonjwa huo, zinahusiana na mishipa ya fahamu iliyo na uhusiano na kiungo kinachotenganisha mapafu na tumbo la chakula. Nyingine magonjwa ya homa ya mapafu (pneumonia).
 
Mbinu zinazosaidia kupunguza kwikwi ni pamoja na; kunywa maji ya baridi kwa njia ya kugugumia, kumtisha mtu mwenye kwikwi japo siyo vyema kumtisha sana na hasa kama hujui afya yake vizuri.
 
Unaweza kumtisha mtu akazimia, hata kupoteza maisha kama alikuwa na magonjwa mengine kama ya moyo. Vitisho visiwe vikali, wala vya kisheria kama kumtishia mtu kumuua, kwani anaweza akakupeleka mahakamani hata kama ulifanya hivyo kwa nia njema.
 
Katika kutibu kwikwi inayotokana na magonjwa mengine ni muhimu madaktari kufanya vipimo na kutibu tatizo husika. Mara nyingi kwikwi inapokaa kwa muda mrefu madaktari watampa mgonjwa dawa za usingizi na zile za kupunguza msongo wa mawazo.
 
KWIKWI (Hiccups)
Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.

Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.

Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.
 
SABABU ZINAZOPELEKEA KUPATA KWIKWI;
• Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
• Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
• Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
• Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
• Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
• Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
 
Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.

SABABU NYINGINE (Rare but serious) ni pamoja na;
• Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)
• Kukusanyika kwa sumu mwilini kama vile sumu ya figo (Uremia)
• Magonjwa ya mapafu kama vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…