Weka Pembeni Tabia Hizi, Ujenge Maisha Ya Mafanikio Unayoyataka
Je, uko tayari kufanikiwa kwa namna yoyote ile? Je, kuna changamoto unazopitia na zinakuzuia kufanikiwa, ingawa wewe kiu yako ni kutaka kuona mafanikio yakiwa kwenye maisha yako? Endapo utamuuliza mtu yeyote swali hili, wengi sana watakwambia, ndio wanataka kufanikiwa, tena utajibiwa kwa haraka sana.
Lakini hata hivyo ni kweli, karibu kila mtu katika maisha yake ana kiu ya kufanikiwa lakini si kila mtu anajua jinsi ya kufanya ili kufanikiwa. Kuna vitabu vingi vimeandikiwa, na makala nyingi zimeandikwa zikieleza kwa wazi nini unapaswa kufanya ili kufanikiwa, na nini ambacho unatakiwa kuepuka sana ili kufanikiwa.
Pamoja na wingi wote wa vitabu na makala hizo za mafanikio, lakini bado watu hawafanikiwi, wamekuwa ni watu wa maisha yale yale, mpaka unaweza ukaa chini ukajiuliza hivi, shida kubwa ipo wapi? Leo kupitia makala haya, nataka nikukumbushe kwa kifupi sana, baadhi ya tabia unazotakiwa uziweke pembeni ili ufanikiwe