Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Habari za asubuhi wakuu.
Namshukuru Mungu kwa Ukuu wake anaojidhihirisha machoni petu kila siku kila saa, hajawahi kutuacha peke yetu kamwe.Hata tupite kwenye magumu ya kukata tamaa,yeye Baba aliye hai hutunyanyua na tunaendelea na mapambano,na tuta shinda tu.
Yeye ni Baba asiye lala...
Yeye ni Baba asiye shindwa...
Mungu akawe nasi sasa na hata milele [emoji120] [emoji120]
 
Usingizi wa uhakika ni jambo jema sana kwa ajili ya afya ya mwili wako. Lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na kujengeka kwa jamii yenye mfumo wa maisha wenye shughuli nyingi, watu wengi hawapati usingizi mzuri.
 
Habari za asubuhi wakuu.
Namshukuru Mungu kwa Ukuu wake anaojidhihirisha machoni petu kila siku kila saa, hajawahi kutuacha peke yetu kamwe.Hata tupite kwenye magumu ya kukata tamaa,yeye Baba aliye hai hutunyanyua na tunaendelea na mapambano,na tuta shinda tu.
Yeye ni Baba asiye lala...
Yeye ni Baba asiye shindwa...
Mungu akawe nasi sasa na hata milele [emoji120] [emoji120]
Amin[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Namkumbuka rafiki yangu mmoja alipata kazi nyingi sana kwenye mtandao. Hivyo ikamlazimu azifanye zote kwa muda mfupi bila kulala wala kula ipasavyo. Matokeo yake ameugua kwa miezi mitatu sasa na bado afya yake haijaimarika kama awali.
 
Hili linatupa umuhimu wa kuchunguza ni nini hasa manufaa ya kulala au usingizi mzuri?

Huimarisha na kuboresha ukuaji wa mwili.
Hujenga na kuimarisha kinga mwili.
Hukuweka katika hali nzuri.
Hukuongezea kumbukumbu.
Hurefusha Maisha.
Huboresha tendo la ndoa.
Huondoa msongo wa mawazo.
 
Punguza mwanga wa rangi ya bluu jioni na usiku

Mwanga huu hupatikana hasa katika vifaa vya kielekroniki kama simu; kompyuta, televisheni n.k. Utafiti unaonyesha kuwa mwanga huu wa bluu hupunguza uzalishaji wa homoni ya “melatonin” ambayo ndiyo hutupa usingizi. Inashauriwa kuepuka kutumia mitandao ya kijaamii au kutazama vitu katika vifaa tajwa hapo juu ili kuboresha usingizi wako.
 
Kaa kwenye mwanga wa kutosha mchana

Unapokaa kwenye mwanga wa kutosha mwili wako utaweza kutambua ni wakati upi umeamka na ni wakati gani wa kulala. Yaani mwili utatengeneza mazoea ya kubaini kuwa sasa ni usiku na ni wakati wa kulala kwani mchana kutwa hukuwa umelala.
 
Epuka matumizi ya Caffeine jioni au usiku

Sokoni leo vipo vinywaji kadha wa kadha vilivyotengenezwa au kuongezewa caffeine. Matumizi Caffeine huamsha na kuchangamsha mwili wako na kuuweka katika hali ya kutojipumzisha. Hivyo matumizi ya caffeine jioni au wakati wa kulala kutakupelekea kutopata usingizi mzuri. Vinywaji vyenye caffeie nyingi ni kama vile kahawa pamoja na baadhi ya soda.
 
Punguza au acha kulala mchana

Mara ngingi unapolala mchana ni sawa na kusema umepunguza usingizi wa usiku. Kama siyo lazima kulala mara kwa mara mchana, basi ni vyema ukajitahidi kutolala ili kukupa usingizi wa uhakika na wa kutosha wakati wa usiku. Kumbuka, hakuna sababu ya kulala mchana wakati una usiku mzima wa kulala.
 
Zingatia ratiba ya kulala na kuamka

Natumaini umewahi kulala zaidi ya muda uliozoea kuamka; na ulipoamka ulijikuta umechoka sana. Vivyo hivyo kwa siku uliyochelewa kulala pia. Hivyo basi, jitahidi kulala na kuamka kwa wakati ili mwili wako uweze kufuata utaratibu ambao umeuzoea. Mwili unapobadilishiwa utaratibu uliouzoea mara kwa mara ni dhahiri utakuonyesha matokeo hasi.
 
Usitumie kilevi/pombe

Kama nilivyoeleza katika hoja ya kwanza, “melatonin” ni homoni muhimu inayotuwezesha kulala. Hivyo basi utafiti uliofanyika umebaini kuwa uzalishaji wa homoni hii huathiriwa na matumizi ya pombe. Pombe ni kinywaji ambacho kimeonyesha kuwa na hasara nyingi katika mwili wa binadamu, hivyo ni vyema ukajitahidi kuepuka matumizi ya pombe.
 
Boresha mazingira ya chumba unacholala

Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wanaopata matatizo ya kulala yanasababishwa na mazingira mabaya ya vyumba vyao vya kulala. Hakikisha unalala kwenye chumba ambacho hakina mwanga mwingi, joto kali, baridi, uhaba wa hewa au kelele.
 
Mambo unayoweza kufanya kuboresha chumba chako:

Zima au punguza mwanga katika chumba chako.
Zima redio, televisheni au kifaa kingine kinachosababisha kelele.
Fungua madirisha ili kuhakikisha unapata hewa yakutosha.
Tawala joto na baridi kwani visipokuwa vya wastani hutoweza kulala vyema – angalau nyuzi joto 20 zinatosha.
Naamini ukizingatia haya utaboresha usingizi wako na kukuwezesha kulala vyema.
 
Usile sana usiku au usile vyakula vizito usiku

Kutokana na watu wengi kuwa na shughuli nyingi wakati wa mchana hushindwa kula vyema mchana; hivyo hupendelea kula sana usiku. Hili sii jambo zuri kwani mwili unakuwa umepumzika wakati wa usiku; hivyo kula sana au kula vyakula vigumu kutapelekea mwili kutumia nguvu kubwa kumeng’enya chakula hicho. Ndiyo maana watu wengi wanaopenda kula sana usiku huamka asubuhi wakiwa wamechoka sana.
 
Back
Top Bottom