Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-13-20-29-41.png
 
Kumlazimisha mtembeleaji kufanya vitu

Ikiwa unalipwa kwa njia ya watembeleaji kubofya picha au kitu fulani kwenye tovuti au blog yako, hakikisha huwalazimishi kufanya hivyo ili upate pesa.

Watembeleaji wakibaini hili hawatakuja tena kwenye tovuti au blog yako kwani wataona kuwa unataka kuwatumia kuzalisha pesa na sio kuwapa kile wanachokihitaji.
 
Kuto kuzingatia lengo

Lengo ni muhimu sana kwenye kufanikisha jambo lolote. Tovuti na blog nyingi hufa kutokana na kukosa lengo; leo unaandika elimu, kesho siasa, keshokutwa habari, siku nyingine udaku, siku nyingine miziki n.k

Huku ni kukosa lengo na kwamwe hutoweza kufanikiwa kama hutoacha kosa hili la kukosa lengo. Bainisha unataka uandike nini, kwa ajili ya nani na kwa ajili ya nini.
 
Kuteka au kumzuia mtembeleaji

Nimeona baadhi ya watu wakifikiri kuwa kumzuia mtembeleaji kuondoka au kumlazimisha kukaa kwenye tovuti au blog zao ndiyo kuzalisha faida zaidi.

Ni kosa kuteka kivinjari au kifaa cha mtumiaji ili asiondoke kwenye tovuti yako.

Hakikisha mtembeleaji mwenyewe anaona sababu ya kuendelea kukaa kwenye tovuti yako na si kwa kumlazimisha.
 
Kuto zingatia kufunguka kwenye vifaa mbalimbali

Hivi leo asilimia kubwa ya watumiaji wa mtandao wanatumia simu za mkononi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha tovuti au blog yako inafunguka vyema kwenye vifaa vyote na si kompyuta pekee.
 
Kutumia web host mbaya

Kuna mahali ambapo taarifa au maudhui ya tovuti fulani hukaa; eneo hili ndilo huitwa web host. Kutokana na ukosefu wa uelewa pamoja na kukwepa gharama watu wengi wamejikuta wakitumia host duni ambazo huathiri tovuti zao kwa kiasi kikubwa.

Kumbuka host mbaya zina virusi, wadukuzi, hazipatikani wakati wote, zina kasi ndogo n.k Unaweza kuzingatia mambo haya wakati wa kuchagua web host

Hakikisha inapatikana wakati wote (Uptime 99.9%)
Hakikisha inaulinzi madhubuti.
Hakikisha inahuduma nzuri kwa wateja (Saa 24).
Hakikisha wana huduma za kisasa na unazozihitaji.
Hakikisha wanaelezwa vyema na watumiaji wengine (Reviews).
Hakikisha gharama na njia zao za malipo zinaeleweka vyema.
Kwa kufanya hivi utakuwa umechagua web host nzuri ambayo haita athiri utendaji kazi wa tovuti yako. Fahamu hili tunapendekeza utumie Smart Host UK ni nzuri sana.
 
Back
Top Bottom