Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tambua bidhaa unazozitumia

Watu wengi hununua na kutumia bidhaa bila kuzifahamu vyema, inawezekana ni kutokana na ukosefu wa elimu au kuishi kwa mazoea. Elewa kila chakula au kinywaji unachotumia kina nini ndani yake.

Vinywaji vingine na vyakula vina viambata ambavyo ni sumu katika mwili wako. Kama siyo lazima kutumia kitu basi kiepuke ili kupunguza kama siyo kuondoa kiwango cha sumu kinachoingia mwilini mwako.
 
Epuka matumizi ya plastiki

Vyombo vilivyotengenezwa kwa plastiki vimetokana na kemikali mbalimbali ambazo nyingine ni hatari kwa afya yako. Matumizi ya vyombo vya chakula vilivyotengenezwa kwa plastiki vinaweza kusababisha kemikali kama vile polymer kuingia mwilini mwako.
 
Hatari huzidi pale ambapo vyombo hivi hutumika kuwekea vyakula vya moto, kwani husababisha kemikali hizi kuyeyuka na kuingia kwa kiasi kikubwa mwilini. Unaweza kutumia vyombo vya kioo au udongo ili kukabiliana na tatizo hili.
 
Epuka matumizi ya pombe

Kama ilivyo kwa vyakula vya viwandani, pombe nyingi hutengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo nyingine ni hatari kwa afya yako. Ili kuondoa na kupunguza kiasi cha sumu zinazoingia mwilini mwako jitahidi kuepuka matumizi ya pombe na kutumia vinywaji vingine kama vile maji.
 
Tumia dawa kwa uangalifu

Dawa zisipotumika vyema zinaweza kuwa sumu hatari mwilini mwako. Epuka kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu. Dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa pia ni dalili za ugonjwa mwingine, hivyo ni vyema kufanya vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa.
 
Pata masaji

Masaji ina manufaa anuwai kwa jili ya mwili wako. Kufanya masaji hukuwezesha kuwa na mtiririko mzuri wa damu katika sehemu mbalimbali za mwili wako.

Damu inaposafiri vyema mwilini itachukua pia sumu zilizojikusanya kwenye mwili na kuzipeleka kwenye viungo kama ini na figo ili kuchujwa na kutolewa mwilini. Hivyo kama unaweza kupata fursa ya kufanya masaji, basi ifanye ili uweze kuondoa sumu mwilini mwako.
 
IMG_2435.jpg
 
Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga amesema pamoja na changamoto zote anazokumbana nazo lakini anafurahi kuona wachezaji wenzake wakiendelea kumwakilisha vizuri na kuiweka timu hiyo kwenye nafasi nzuri kiasi.
Ngassa amesema sare na ushindi wanaopata katika baadhi ya mechi zimekuwa zikimpa matumaini ya kufanya vizuri endapo atatulia na kujipanga kwa ajili ya kupandisha kiwango chake kwenye kikosi cha Simba.
 
Mabingwa watetezi Ligi Kuu Yanga SC Jumamosi jioni waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 12 baada ya kucheza mechi sita na kupanda juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa wastani wa mabao, sasa wakilingana kwa pointi na Azam FC ambayo imelazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui mjini Shinyanga.
 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, aliyesaidiwa na washika vibendera Joseph Masija na Julius Kasitu pamoja na Jamada Ahmada mezani, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 40 aliyemhadaa beki juma Nyosso na kumchambua kipa mkongwe Juma Kaseja, kufuatia pasi nzuri ya mshambuliaji mwenza, Ibrahim Hajib ambaye naye alipasiwa na Gardiel Michael.
 
Yanga wakaendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa Kagera Sugar baada ya bao hilo, lakini Kaseja alisimama imara kuondosha hatari zote hadi filimbi ya kuugawa mchezo ilipopulizwa.
Na mara baada ya kuanza tu kwa kipindi pili, Yanga wakafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 47 lililofungwa na Ajib, baada ya kupewa pasi nzuri na Chirwa.
 
Wakati Yanga wakiwa kwenye furaha ya kuongeza bao wakashitukizwa kwa bao la Jaffar Kibaya dakika ya 52 aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Venance Ludovic.
Bao hilo likazidi kuuchangamsha mchezo, Yanga wakisaka bao la tatu na Kagera Sugar wakitafuta bao la kusawazisha, lakini walikuwa ni wana Jangwani waliofanikiwa kuulinda ushindi wao wa ugenini.
 
Jurgen Klopp ameziponda mbinu za Jose Mourinho wakati Manchester United ikipata sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool Jumamosi.
United kwa kiasi fulani walicheza kwa kujihami mechi hii, mshambuliaji Romelu Lukaku akigusa mpira mara 22 tu dakika zote alizocheza.
 
Back
Top Bottom