Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zabibu ni matunda matamu yanayopendwa yakiwa na faida nyingi kiafya kwa mwili. Kuna zabibu za rangi ya kijani, nyekundu na rangi kama nyeusi. Unaweza kula zabibu kama matunda, zabibu zilizokaushwa (raisin) au kama juisi pia. Zabibu hutumikana sana kutengeneza mvinyo (wine), sehemu mbalimbali duniani. Faida za zabibu kiafya, hujumuisha kusaidia kuondoa kukosa choo,
 
mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri, kupunguza uchovu/machofu, na kuzuia mtoto wa jicho pia. TUVITAMBUE VIRUTUBISHO VILIVYOPO NDANI YA ZABIBU Kila gramu 100 za zabibu zina wastani wa virutubishi vifuatavyo; Nishati kilokaro 69 Wanga gramu 18.1 Sukari gramu 15.48 Kamba lishe gramu 0.9 Mafuta gramu 0.16 Protini gramu 0.72 ZABIBU PIA ZANA VITAMIN ZIFUATAZO:
 
Vitamini B1, B2, B3, B5, B6, B9 Vitamini C Vitamin E Vitamin K LAKINI PIA ZABIBU ZINA MADINI: Kalsiamu miligramu mg 10 Chuma miligramu 0.36 Magneziamu miligramu 7mg Manganizi miligramu 0.71 Sodiamu miligramu 2 Potasiamu miligramu 191 Fosforasi miligramu 20 TUANGALIE SASA FAIDA ZAKE KIAFYA:
 
Ulaji wa zabibu katika mlo wako, una faida nyingi kiafya, zikiwemo: Kutibu Pumu Zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu katika njia ya hewa, na hivyo zinapunguza utokeaji wa pumu. Huimarisha Mifupa Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi katika zabibu, ambapo madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya.
 
Back
Top Bottom