Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zabibu huongeza nitric oxide katika damu, ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kujirundika/kujikusanya katika mishipa ya damu, na ina kampaundi za flavonoids aina ya resveratrol na quercetin, ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Yote haya, husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo, na shinikizo la damu
 
KUPUNGUZA LEHEMU (CHOLESTEROL) Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu kwenye damu. Zina kampaundi kama pterostilbene, ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyomo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins, hizi hupunguza unywonyaji wa lehemu, kutoka kwenye utumbo. KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA SARATANI Kama nilivyokwambia mwanzo, kampaundi zinazopatikana katika zabibu kama resveratrol, husaidia kuondoa sumu,
 
zinazoweza kuleta saratani mwilini. Baadhi ya kampaundi nyingine huzuia seli za saratani kukua, na kuzaliana; zinaimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi pia, kama kuzuia choo kigumu, homa, na kuongeza damu. MUHIMU Hakikisha unazikosha vizuri zabibu zako kwa maji safi ya moto, kabla ya kuzila.
 
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…