Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
* Kausha uso wako kwa taulo safi.
* Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dakika kama 3 mpaka 5.
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
* Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.
* Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.