Tezi dumeni ile ambayo seli zisizo za kawaida hukua katika tezi ya prostate iliyopo katika mfumo wa uzazi wa mwanaume. Kwa walio wengi, ukuaji wa saratani hii huwa ni wa taratibu ingawa kwa wengine yaweza kukua kwa haraka. Saratani yaweza kusambaa katika sehemu nyingine za mwili,hususan katika mifupa na tezi zinazo husika na kinga ya mwili (lymph nodes). Mara nyingi saratani ya tezi ya prostate huwa haionyeshi dalili yeyote katika hatua za awali. Saratani hii imeonekana kuwaathiri zaidi wanaume wenye asili ya Afrika na Caribbean lakini haijulikani ni kwa sababu gani.