Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ugonjwa huu ambao hauko katika kundi la magonjwa ya zinaa, lakini kufanya ngono wakati mwingine husababisha kuambukizwa kwa ugonjwa huu

Dalili za UTI hutofautiana kulingana na sehemu ya njia ya mkojo iliyoathirika.
Jedwali
Sehemu iliyoathirika
Dalili
Figo

Kichefuchefu.
Kutapika.
Maumivu ya mgongo wa juu.
Homa kali.
Kutetemeka na kusikia baridi
Kibofu

Damu katika mkojo.
Maumivu ya nyonga.
Maumivu chini ya kitovu.
Kukojoa mara kwa mara na kupata maumivu wakati wa kukojoa.

Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu (urethra)

Mkojo wa kuunguza wakati wa kukojoa(maumivu njia ya mkojo)
 
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8]

[emoji445][emoji443][emoji444][emoji443][emoji445][emoji443][emoji444]
I choose to love you in silence…
For in silence I find no rejection,

I choose to love you in loneliness…
For in loneliness no one owns you but me,

I choose to adore you from a distance…
For distance will shield me from pain,

I choose to kiss you in the wind…
For the wind is gentler than my lips,

I choose to hold you in my dreams
For in my dreams, you have no end

[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
 
Siyo mara zote ambazo mtu hupata dalili za ungonjwa huu, lakini zinapotokea huwa ni kama ifuatavyo:- Kujisikia haja ya kukojoa mara kwa mara, kusikia maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara mkojo kidogo, mkojo wa rangi ya mawingu mawingu, mkojo mwekundu au pink, pia wa rangi ya brauni, mkojo unaotoa harufu, maumivu ya nyonga kwa wanawake na maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wanaume. Endapo utakuwa na dalili hizo zilizotajwa awali ni vyema kupata ushauri wa daktari.
 
Uambukizi wa njia ya mkojo hutokea kama bakteria wataingia katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu, na huzaliana na kuongezeka katika kibofu. Ingawa bakteria hawa waweza kuishi katika kibofu bila kuleta madhara, lakini wakati mwingine kinga ya mwili hushindwa kufanya kazi ipasavyo na uambukizi hutokea. Uambukizi unapotokea ndipo mgonjwa anaweza kuona dalili mbalimbali tulizoziona awali.
 
Kama tulivyoona awali mara nyingi ugonjwa huu huwaathiri zaidi wanawake na sababu kubwa ikiwa ni ya maumbile.
Uambukizi katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu (Infection of the urethra)-Aina hii ya UTI hutokea endapo bakteria wanaopatikana tumboni watasambaa kutoka njia ya haja kubwa na kuingia katika mrija wa mkojo. Na kwa kuwa mrija wa kutoa mkojo uko karibu uke mwanamke anaweza pia kuambukizwa UTI kwa kufanya ngono, ambapo vijimelea kama gonococcus na chlamydia vinaweza kusabisha aina hii ya UTI.
 
Uambukizi katika kibofu- Aina hii ya UTI mara nyingi husababishwa na bakteria aina ya E coli, bakteria hawa hupatikana tumboni.Maumbile ya uke kuwa karibu ya njia ya aja kubwa huchangia sana bakteria hawa kuweza kuingia kwa urahisi katika njia ya mkojo na kusababisha uambukizi.
 
Walio katika hatari ya kupata ugonjwa.
Wagonjwa walioingiziwa mpira wa kusaidia kutoa mkojo(catheter) huwa katika hatari kubwa ya kupata UTI. Hii inajumuisha wagonjwa waliolazwa, wenye matatizo ya magonjwa ya fahamu na hawawezi kutoa mkojo, pia wagonjwa waliopooza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…