Ununuzi mwingi zaidi unaendelea kufanywa mtandaoni. Google husaidia wateja kupata bidhaa kwa njia kadhaa, na, ingawa hatudhibiti maudhui yaliyo mtandaoni, tunataka kuwasaidia wateja kununua kwa usalama mtandaoni. Idadi kubwa ya ununuzi mtandaoni hukamilishwa bila matatizo yoyote, lakini wakati mwingine kuna hatari, na hii ndiyo sababu tumeanzisha ukurasa huu ulio na vidokezo na zana muhimu unazoweza kutumia katika ununuzi wako mtandaoni.
Ikiwa bei inaonekana rahisi sana ...: kuwa mwangalifu. Linganisha bei unayoona na bei ya bidhaa sawa zinazouzwa mahali pengine. Ikiwa bei inatofautiana sana, kuwa mwangalifu - hakikisha umemchunguza muuzaji na umuulize maswali kuhusu hali ya bidhaa hiyo.
Tovuti inayouza bidhaa ambazo zina punguzo kubwa au iliyoandikwa kwa sarufi mbovu na makosa ya tahajia, na inayotumia picha zenye ubora wa chini za tovuti rasmi ya mmiliki wa bidhaa, huenda inauza bidhaa bandia. Kuwa mwangalifu pia, kwa sababu tovuti nyingine zinazouza bidhaa bandia huiga tovuti ya mmiliki wa bidhaa halisi kwa kuiga miundo na kutumia picha sawa au kutumia jina la kikoa linalojumuisha bidhaa hiyo.
Chunguza wauzaji wasiojulikana: Ikiwa hujawahi kununua kutoka muuzaji fulani, chunguza mapema ili uhakikishe kuwa yeye ni halisi. Kwa mfano, pata maelezo zaidi kuhusu historia ya biashara yake na utafute mtandaoni maoni ya wanunuzi wengine wanaomfahamu muuzaji huyu.
Wauzaji halali kwa kawaida hutoa anwani ya mawasiliano unayoweza kutumia ikiwa una maswali au matatizo yoyote wakati wa kununua, ambayo inaweza kujumuisha mahali halisi wanapopatikana, nambari ya simu, au barua pepe. Tovuti nyingi zinazouza bidhaa bandia zitakuwa na URL zinazofanana na zile rasmi, ambazo zinaweza kujumuisha maneno kama [bidhaa]onsale.com au [bidhaa].com rasmi. Kuangalia rekodi ya WhoIs ya tovuti hii ni njia moja inayoweza kumtambua mmiliki wa kikoa.
Tumia njia ya malipo iliyolinda wanunuzi: Mara nyingi, kampuni ya kadi za mikopo hudhibiti dhima yako kwa ununuzi wa mtandaoni wakati kuna ulaghai. Mifumo mingine ya malipo ya mtandaoni haishiriki nambari nzima ya kadi yako ya mkopo kwa wauzaji ili kukupa ulinzi zaidi.
Soma maelezo yaliyoandikwa kwa herufi laini: Kabla ya kununua, hakikisha unafahamu njia ya usafirishaji wa bidhaa, udhamini, na sera ya kurejesha bidhaa. Maduka mengine hurejesha fedha zote, na mengine hutoza ada ya kurejesha bidhaa na hukubali tu kubadilisha bidhaa.
Weka rekodi ya ununuzi: Kuwa na nakala ya dijitali au ya karatasi ya ununuzi mkubwa, kunaweza kukusaidia ikiwa utahitaji kurejesha bidhaa au kuwasilisha malalamiko ya ada zisizoruhusiwa zilizotozwa kwenye akaunti yako.
Epuka tovuti zilizovamiwa na kuwa makini kuhusu sehemu ya anwani ya kivinjari. Ukibofya kiungo kisha uelekezwe kwingine haraka, huenda tovuti hiyo imevamiwa na ina programu hasidi. Programu hasidi, kama vile virusi, vijidudu, na virusi vya Trojan, zinaweza kusakinisha programu zisizofaa kwenye kompyuta yako bila idhini yako.
Tovuti nyingine zilizovamiwa hazitakuelekeza kiotomatiki kwenye ukurasa mwingine, lakini zinaweza kuwa na maudhui taka au yasiyo muhimu kwenye ukurasa huo. Kuwa makini kuhusu sehemu ya anwani ili kuhakikisha kwamba umeelekezwa kwenye kiungo ulichobofya ni mojawapo ya njia za kutahadhari.
Andika anwani ya tovuti nyeti katika sehemu ya anwani ya kivinjari chako: Usiingie katika akaunti nyeti kwa kubofya kiungo au kunakili na kupachika anwani yake. Badala yake, andika mwenyewe anwani ya wavuti. Lakini hakikisha kwamba unaandika anwani sahihi; baadhi ya tovuti bandia hufanana na tovuti halisi, lakini huundwa kwa madhumuni ya kuhadaa ili kupata maelezo ya akaunti yako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.