Tumia nenosiri ndefu linalojumuisha nambari, herufi na alama
Nenosiri lako likiwa refu, basi itakuwa vigumu kulikisia. Hivyo lifanye neosiri lako refu ili usaidie kuweka maelezo yako salama. Kuongeza nambari, alama na mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo hufanya iwe vigumu zaidi kwa wanaotaka kuchungulia au wengine, kukisia au kujua nenosiri lako. Tafadhali usitumia ‘123456’ au ‘nenosiri,’ na jiepushe na kutumia maelezo yanayopatikana hadharani kama vile nambari yako ya simu, katika manenosiri yako. Si halisi, wala si salama!