Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jaribu kutumia fungu la maneno ambalo ni wewe tu unayelifahamu

Njia moja ni kufikiria fungu la maneno ambalo ni wewe pekee unayelijua, na ulihusishe na tovuti fulani kukusaidia kulikumbuka. Kwa barua pepe yako unaweza kuanza kwa "Rafiki yangu Tom hunitumia barua pepe ya kufurahisha mara moja kwa siku" na kisha utumie nambari na herufi ili kuliunda upya. “RayT;Hu&Bp🙂” ni nenosiri lenye herufi tofauti. Kisha rudia utaratibu huu kwa tovuti zingine.
 
Ikiwa utasahau nenosiri lako au ushindwe kuingia kwenye akaunti, unahitaji njia ya kurudi kwenye akaunti yako. Huduma nyingi zitakutumia barua pepe katika anwani ya barua pepe ya kurejesha uwezo wa kufikia akaunti ikiwa unahitaji kuweka nenosiri jipya, hivyo hakikisha barua pepe yako ya urejeshi imesasishwa na bado unaweza kuifikia akaunti hiyo.
 
Wakati mwingine unaweza pia kuongeza nambari ya simu kwenye wasifu wako ili utumiwe msimbo wa kuweka nenosiri jipya kupitia SMS. Kuwa na nambari yako ya simu ya mkononi kwenye akaunti yako ni mojawapo ya njia rahisi na za kuaminika za kusaidia kuweka akaunti yako salama.
 
Kwa mfano, watoa huduma wanaweza kutumia nambari yako ya simu kutoa changamoto kwa wale wanaojaribu kuingia kwenye akaunti yako bila idhini, na kukutumia msimbo wa uthibitishaji ili uweze kuingia kwenye akaunti yako endapo utashindwa kuifikia. Kupatia Google nambari ya simu ya urejeshi hakutakufanya uingizwe kwenye orodha za mauzo au upigiwe simu na wanaofanya uuzaji kupitia simu.
 
545aece62478804025942eaa52d5b4e6.jpg
 
Simu yako ya mkononi ni mbinu salama zaidi ya kuthibitisha utambulisho kuliko anwani yako ya barua pepe ya urejeshi au swali la usalama kwa sababu, tofauti na mbinu hizo zingine mbili, una umiliki halisi wa simu yako ya mkononi.
 
Hata hivyo, ikiwa hutaki au huwezi kuongeza nambari ya simu kwa akaunti yako, tovuti nyingi zinaweza kukuuliza uchague swali la kuthibitisha utambulisho wako endapo utasahau nenosiri lako. Ikiwa huduma unayotumia inakuruhusu ujitungie swali lako mwenyewe, jaribu kupata swali lenye jibu ambalo ni wewe pekee unayelijua na si kitu ambacho umechapisha hadharani au umeshiriki kwenye mitandao jamii.
 
Back
Top Bottom