Hata hivyo, ikiwa hutaki au huwezi kuongeza nambari ya simu kwa akaunti yako, tovuti nyingi zinaweza kukuuliza uchague swali la kuthibitisha utambulisho wako endapo utasahau nenosiri lako. Ikiwa huduma unayotumia inakuruhusu ujitungie swali lako mwenyewe, jaribu kupata swali lenye jibu ambalo ni wewe pekee unayelijua na si kitu ambacho umechapisha hadharani au umeshiriki kwenye mitandao jamii.