Apps tatu muhimu za Android kwa ajili ya kusomea vitabu.
Smartphones zimebadili sana mifumo ya maisha yetu. Tofauti na simu za kawaida (features phones) ambazo kazi yake kubwa ni kupiga, kupokea simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms). Smartphones zina mambo mengi sana unayoweza kufanya ndani yake. Katika nyakati hizi za utandawazi pamoja na mabadiliko ya kidigitali, si lazima tena kununua vitabu vikiwa katika mfumo wa karatasi (hard copy).
Unaweza nunua vitabu vikiwa katika mfumo wa digitali (digital edition/soft copy) na kusoma popote pale uendapo katika smartphone/tablet yako. Lakini, kuweza kufanikisha suala hili ni lazima uwe na application ambayo itasoma aina hii ya vitabu katika kifaa (device) chako. Vitabu, majarida na nyaraka nyingine huwa katika mifumo ya pdf, epub au mobi. Tuangalie apps tatu rahisi na muhimu kutumia katika kuwezesha suala hili.
App hii inapatikana katika PlayStore kama ya bure ikiwa na features chache za msingi(lite) na pia kama utahitaji kutumia features zote (premium version) itabidi kulipia dola $5.87 za Kimarekani
(sawa na takribani Tsh. 10,000). Uzuri wa apps za Android zinazohitaji malipo katika ununuzi wake huweza patikana bure kabisa kwa njia ambayo wengi tunaifahamu kama pirating, apps hizi huwa zipo cracked, hii ina maana ya kwamba features zote ambazo zinafunguka kwa kuhitaji malipo utazikuta zikiwa tayari zimefunguliwa na tayari kutumika bila kikwazo chochote.
App hii ina features nyingi sana. Kuanzia muonekano wake mpaka vitu ilivyosheheni. Inaweza kusoma mafaili yaliyo katika mfumo wa pdf, epub, epub2 na epub3. Hii inakuwezesha kusoma aina mbalimbali ya mafile ukitumia app moja tu.
Ina uwezo wa kuchagua ukubwa kava la nje la kitabu (thumbnail) pale lionekanapo katika kabati (shelf) la vitabu vyako, ina features nyingi katika kuwezesha kupangilia maktaba yako.
Inakuwezesha kuchagua rangi ya nyuma (background color) unaposoma kitabu. Unaweza chagua themes ambazo zinakuja na app (pre-installed) au kutengeneza ya kwako kulingana na vile unavyopendelea.
Inakuwezesha kusoma kwa kutumia night mode ambayo huleta muonekano wa nyuma (background color) ambao una rangi nyeusi ili kuepusha kuumia macho hasa unaposoma kitabu nyakati za giza.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.