Elewa vizuri sana mahitaji yako au tatizo lako – Unataka kuwa na ngozi laini, unataka kuondoa tatizo fulani katika ngozi yako, unataka kuboresha rangi ya ngozi yako nk
Elewa vizuri sana mahitaji yako au tatizo lako – Unataka kuwa na ngozi laini, unataka kuondoa tatizo fulani katika ngozi yako, unataka kuboresha rangi ya ngozi yako nk
Elewa vizuri sana aina ya ngozi yako – ni kavu au ya mafuta au ya kawaida au mchanganyiko? Hii itakusaidia kujua vipodozi ambavyo utaweza kutumia na visikuletee matatizo mengine.
Kwa mfano kama ngozi yako ni ya mafuta ila ukaanza kutumia losheni kwa ajili ya ngozi kavu ili kuondoa madoadoa unaweza ukatokwa na vipele, mafuta kuongezeka na kadhalika
Baada ya hapo kilichobaki ni kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako na vyenye uwezo mkubwa zaidi wa kukidhi mahitaji yako au kuondoa tatizo lako ndani ya muda mfupi iwezekanavyo
Nunua vipodozi vyako kutoka katika maduka ya kuaminika. Usinunue vipodozi ovyo, hautapata matokeo mazuri na utapata madhara mbalimbali pamoja na kupoteza pesa zako nyingi
Matokeo mazuri yanahitaji utumie vipodozi vizuri na uvitumie kama inavyotakiwa. Ukikosea chochote kati ya hivyo utachelewa kupata matokeo unayoyataka au hautapata matokeo kabisa.
Kama unasumbuliwa na harufu mbaya kwapani hakikisha usafi wa hali ya juu kwa kunyoa nywele za kwapani mara kwa mara na kuoga kwa kutumia sabuni zenye dawa zinazosaidia kudhibiti bakteria. Tumia sabuni kama vile protex, dettol, rungu medicated soap, family medicated soap, protector nk
Baada ya kuoga na kuvaa unaweza kujipulizia au kujipaka kipodozi mahususi kwa ajili ya kudhibiti harufu ya jasho au mwili ambacho huitwa Deodorant. Kuna deodorant za kupaka kwapani moja kwa moja na zile za kupulizia kwenye nguo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.