Asidi hiyo huwa katika hali ya majimaji na hutulia tumboni. Kukiwa na hitilafu katika uzalishwaji wake inaweza kuzalishwa kwa wingi zaidi na kiasi huweza kubadilika na kuwa katika mfumo wa hewa (gesi) ambayo hujaa tumboni na kuweza kupanda hadi kwenye njia ya juu ya chakula na kufika kooni.
Kiungulia hutokea pale gesi hiyo inapopanda na kuja kooni ambapo hutufanya tuhisi kama tunaungua, na tumbo kujaa gesi hutokea pale gesi hiyo inapoongezeka na kujaa tumboni.
Kiungulia hutokea pale gesi hiyo inapopanda na kuja kooni ambapo hutufanya tuhisi kama tunaungua, na tumbo kujaa gesi hutokea pale gesi hiyo inapoongezeka na kujaa tumboni.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo vinaweza kusababisha au kuongeza uzalishwaji wa asidi nyingi tumboni na kuweza kupelekea au kuongeza matatizo ya kiungulia na tumbo kujaa gesi
Baadhi ya vyakula na viungo kama vile vyakula vya mafuta mengi, vyakula vilivyokaangwa, nyanya, vitunguu, matunda jamii ya machungwa/machenza, vitunguu swaumu nk
Maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa