Kwa malaria ya kawaida unaweza kujadili na daktari dawa unayoipenda na unayoweza kuinunua kati ya Mseto (ALU), Duo-Cotexin, Artequick au D-Artepp. Una haki ya kuchagua dawa, lakini ni muhimu pia kufuata ushauri wa daktari.
Baada ya kutumia dawa za malaria unaweza kurudia vipimo na kupata ushauri wa daktari ili kujua kama umepona vizuri na jinsi ya kuishi vizuri bila malaria.