Dk Mandai anasema, kwa kawaida ugonjwa wa kisukari cha mimba humpata mwanamke mjamzito kipindi cha kuanzia wiki 24 na kuendelea.
Hata hivyo, ugonjwa huu huwa haudumu kwa muda mrefu, kwani hupotea mara baada ya mama mjamzito kujifungua. Pi
kisukari hiki huwa na uwezokano wa kuendelea kwa kubadilika kuelekea katika hatua nyingine tofauti kabisa.
Aidha, Dk Mandai anaeleza kuwa, tatizo hili limekuwa likiwaathiri wanawake walio wengi kutokana na kutokuwa na tabia ya kupima kisukari cha mimba kipindi cha ujauzito. Hali hii huwapelekea kutofahamu hali zao kiafya kuhusu kisukari cha mimba.
Aidha, uchunguzi wa wataalam unaonesha kuwa mjamzito anayeongezeka uzito wa gramu 403.70 kwa wiki yupo hatarini kupata kisukari cha mimba, lakini yule anayeongezeka uzito wa chini ya gramu 272.15 kwa wiki, hayuko hatarini kupata ugonjwa huu.