Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b97f1558e17270d9cc57109719cc4cda.jpg
Unasema
 
Mechi ya mwisho Simba ilicheza kwenye uwanja huo wa Sokoine dhidi ya wenyeji wengine Mbeya City, na kushinda bao 1-0, bao ambalo limelalamikiwa na wenyeji Mbeya City wakidai mfungaji Shiza Kichuya alikuwa amezidi, lakini Tanzania Prisons wao mechi ya mwisho walipata sare ya ugenini kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba, baada ya kwendanao sare ya kufungana 1-1.
 
Matokeo hayo yanaufanya mchezo wa kesho kuwa mgumu na wenye ushindani wa aina yake kwani kila upande umejidhatiti kuhakikisha unapata pointi tatu na kuendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo imeonekana kuwa ngumu na ushindani mkubwa msimu huu.
 
Simba mbali na kupewa nafasi kubwa ya ushindi kutokana na ubora wa kikosi chake lakini itawabidi kucheza kwa tahadhari kubwa kwani msimu uliopita waliweza kuacha pointi tatu kwenye uwanja huo mbele ya Maafande hao mabao ya mshambuliaji Peter Hangaya, ambaye alimtungua kipa Mu Ivory Coast Vicent Angban na Simba kupoteza mchezo kwa mabao 2-1.
 
Uwepo wa mshambuliaji Mohamed Rashid mwenye mabao sita kwenye kikosi cha Prisons, kunapaswa Simba, kucheza kwa tahadhari kwani vinginevyo wanaweza kujikuta wanapoteza mchezo huo kwamara ya kwanza msimu huu na kuwapa mwanya wapinzani wao Yanga kuongoza ligi endapo watashinda mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Mbeya City.
 
Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kikosi kamili kisicho na majeruhi lakini ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Emmanuel Okwi na John Bocco wakati kwenye eneo la kiungo Nyarwanda Haruna Niyonzima na Jonas Mkude wakitarajiwa kuzuia na kuanzisha mashambulizi ya timu hiyo .
 
Back
Top Bottom