CHUO KIKUU CHA KWANZA HAPA DUNIANI
Duniani kuna vyuo vingi vikuu na maarufu kama vile Oxford, Bradford, Cambridge, Texas nk. lakini watu hawajui ni chuo gani kikuu cha kwanza apa duniani, Jibu in kwamba chuo kikuu cha Bologna au University of Bologna a.k.a (UNIBO) ndio chuo kikuu cha kwanza kujengwa hapa duniani. Chuo hiki kinapatikana katika taifa la UITALIANO (Italy) chuo hiki kilianzishwa mnamo mwaka 1088 hii iliuwa mwishoni mwa karne ya 11. Hiki ndicho chuo cha kwanza kuitwa University hapa duniani, na hili jina lilipatikana baada ya mjadala mrefu baina ya wanafunzi na wakufunzi wao ambapo kauli mbiu (Motto) wa chuo hicho ulikuwa ni Alma mater. Katika kipindi hiki ndipo elimu ya siasa ilianza kuibuka na kukua kule barani Ulaya na chanzo cha siasa ilikuwa ni hiki chuo na uhusiano baina ya mataifa ulianza kuibuka. Na wanasheria wa kwanza wa ngazi ya juu walitoa atika chuo hiki mwaka 1158 wakitunukiwa shaada ya udhamivu. Chuo hiki kilianzishwa kikiwa department 33, school 11 na fulcuty 23 ambazo ni:
• School of Agriculture and Veterinary Medicine
• School of Economics, Management and Statistics
• School of Engineering and Architecture
• School of Foreign Languages and Literature, Interpretation and Translation
• School of Law
• School of Letters and Cultural Heritage
• School of Medicine and Surgery
• School of Pharmacy, Biotechnologies and Sport Sciences
• School of Political Sciences
• School of Psychology and Education Sciences
• School of Sciences
Chuo hiki ndicho kilichosaidia mapinduzi ya viwanda kaitia bara la Ulaya mnamo karne ya 18 chini ya mainjinia waliobobea wakiongozwa na Luigi Galvani sambamba na akina Alessandro Volta, Benjamin Franklin na Henry Cavendish. Kutoana na mchango mkubwa wa chuo kikuu hiki mnamo mwaka 1888 chuo kilifanya Jubilee ya 8, ya kutimiza miaka 800 ambayo ilihudhuriwa na wakuu wa vyuo vyote vikuu hapa duniani kwa wakati huo na chuo hicho kilitunukiwa nishani ya heshima ya chuo mama cha dunia “the mother of all universities”.