Sauti kubwa zilisikika Zlatan Ibrahimovic akimkumbatia Anthony Martial na kuingia dimbani kwa mara ya kwanza baada ya miezi saba, akinyoosha mikono, kichwa kikiangalia chini. Aliinua kichwa chake baada ya umbali wa yadi chache, kisha akamtazama Romelu Lukaku, akamnyooshea kidole namba tisa wa Manchester United na kumwelekeza kutoka katikati ya dimba. "Upande wa kulia," alionekana dhahiri akifunua kinywa chake.