Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa namna hiyo, Ibrahimovic alikuwa amerudi. Na Lukaku alihisi tofauti. Ambako Jose Mourinho alimwanzisha kipindi cha pili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Newcastle United Jumamosi Marcus Rashford akicheza pembeni mwa Lukaku katika mfumo adimu wa 4-4-2, yote hayo ni kumpa nafasi Zlatan kucheza kwa kujitanua dakika 15 za mwisho za mechi.
 
Hadi Msweden huyo anarejea kazini wikiendi, Lukaku alikuwa mchezaji asiyehamishika akiwa mstari wa mbele kwenye mashambulizi United. Kama ilivyokuwa kwa Ibrahimovic msimu uliopita, na mchezaji huyo wa zamani wa Everton alipewa jukumu hilo na meneja wake kabla ya watu kuanza kuzungumzia kiwango chake wiki za hivi karibuni. Lakini sasa wana miamba miwili mikubwa, wapiganaji hasa ambao kila mmoja atakuwa na jukumu lake, lakini hakuna ishara kwamba Zlatan atapewa jukumu jipya.
 
Ni adimu sana Ibrahimovic kucheza pembeni au kucheza nyuma ya mchezaji mwingine katika kipindi chake cha soka. Kila alipokwenda, mataji yamekuwa yakimfuata. Aliongea mara moja kabla ya kurejea dimbani wikiendi iliyopita kuhusu uwezo wake kufanya majukumu ya namba 10 aliyopewa, lakini ukweli ni kwamba alikuwa akijivunia jezi hiyo ambayo imewahi kuvaliwa na watu maarufu kama Pele, Diego Maradona na Lionel Messi katika nyakati zao tofauti badala ya kuzungumzia nafasi ya kucheza kama namba inayohusiana na jezi hiyo.
 
Ni Barcelona pekee ambako mchezaji huyo anayejiita mwenyewe simba hakuendekezwa na kupewa nafasi ya kucheza mbele na kati, na uhusiano wake na Pep Guardiola kwa ghafla ukawa mchungu kutokana na uamuzi wa kocha huyo kumfanya Lionel Messi mshambuliaji mkuu badala ya Ibra.
 
Kwingine kote amewalazimisha watu kama David Trezeguet, Adriano, Alexandre Pato na Edinson Cavani kucheza nafasi tofauti na asili yao na umahiri wake umemsaidia kukusanya vikombe vya ligi mbali mbali katika bara la Ulaya. Lakini pia alicheza vizuri pembeni mwa wachezaji mahiri zaidi ambao waliimudu vema namba 10 kama Alessandro Del Piero, Clarence Seedorf na Javier Pastore.
 
Zlatan anafahamika kwa umahiri wa kujituma na kuhamasisha mchezo, lakini mbinu sehemu kubwa ya mbinu zake ni kucheza kama mshambuliaji wa kati kuliko uwezo wa kutimiza majukumu ya kiungo mshambuliaji au straika wa pili kama anavyotakiwa kuwa nambari 10.
 
Hii haimaanishi kwamba Lukaku hatapata nafasi nyingine katikati kushambulia kwa sababu mfungaji wa mabao 28 msimu uliopita amerudi. Kwa kuanza, ataendelea kucheza kama namba tisa kwa muda ambao Ibrahimovic anaendelea kupona vizuri huku akitarajiwa zaidi kucheza kutokea benchi.
 
Amepona kabisa lakini sasa hatumtegemei kuwa tayari kucheza dakika zote 90 au kucheza mechi mfululizo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma," Mourinho alimwongelea nyota huyo wa miaka 36 Jumanne kuelekea mechi za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basel ambako United wataweza kutinga hatua ya 16-Bora, sare itapendeza. "Sasa anahitaji kurejea kwenye kiwango chake, uzima wake, kujiamini kwake, ushapu wake, kila kitu chake."
 
Pamoja na yote katika baadhi ya mechi Mourinho anaweza kuamua kuchezesha washambuliaji wawili mbele, na meneja huyo amesisitiza kuwa wanaweza kucheza pamoja ili kuipa mafanikio timu. "Ni rahisi, wachezaji bora wanaweza kucheza pamoja. Tatizo ni pale tu wachezaji wanapokuwa si wazuri, lakini kwa wachezaji bora ni rahisi kwao kucheza pamoja."
 
Inaaminika kuwa United watafaidika ikiwa Mbelgiji huyo atachezeshwa sehemu tofauti na kati. Wakati huo pia United wana wachezaji lukuki ambao wanaweza kucheza pembeni ikiwa ni pamoja na Rashford, Martial, Juan Mata, Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard, shauku ya kuwa na Lukaku XI inaeleweka.
 
Na mwenendo wake wa hivi karibuni katika kiwango kisicho na tofauti vinaashiria kuwa anahitaji kufanya kazi ya ziada kupata magoli, kwa hiyo kusogezwa pembeni kidogo kunaweza kuongeza weledi wake kwani atalazimika kucheza zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…