Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ambaye nchi yake ilikuwa kimbilio la Mnangagwa wakati alipotimuliwa katika nafasi ya makamu wa rais hakuhudhuria sherehe hizo.
“Nitalinda na kukuza haki za watu wa Zimbabwe na kwamba, nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote na nitaheshimu haki za Zimbabwe na raia wake,” amesema katika kiapo hicho.