Na pia, naweza kusema juhudi hizo ni sawa na usemi wa mababu usemao chozi la mama haliendi bure, kwani wapo watu wanaoziona na sasa wanaamua kujitoa kwa moyo wa dhati kusaidia adhima hiyo itekelezeke. Nasema hivyo kwasababu hivi karibuni Serikali ya China kwa kupitia Balozi wake hapa nchini, Wang Ke ilisema itaendela kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu.