Kuzidi kuongeka kwa sebum kutoka kwenye sebacious glands na seli zilizokufa kutajenga msukumo kwenye seli zinazokizunguka kijitundu cha kinyweleo. Msukumo ukiwa mkubwa wa kutosha, kuta za kijitundu hupasuka na mafuta kupenya kwenye ngozi ya karibu
Kwa sababu mafuta haya yana uwingi wa bakteria wa P.acnes, ngozi hii inayozunguka kijitundu hushambuliwa na bakteria hawa na kuifanya ngozi hiyo kuwa na uvimbe nwekundu (pimples). Hali hii
kiutaalamu huitwa inflammatory papule.
Wakati mwili unapambana na bakteria wa P.acnes, chembechembe nyeupe za damu ambazo ni sehemu ya kinga za mwili, hujazana na kutunga usaha katika vijitundu vya vinyweleo. Kwa sababu ambazo bado hazijafahamika vizuri kisayansi, chunusi nyingine hutunga usaha wakati nyingine hazitungi.
Wakati mwingine mafuta na bakteria wanaposambaa kwenye ngozi inayozunguka kijitundu, maambukizi husambaa eneo kubwa na huelekea chini zaidi ndani ya ngozi na kusababisha vijinundu (nodules or cysts) na makovu. Vijinundu hivi huleta maumivu makali na haviponi kwa urahisi.
Chunusi pia hushambulia watu wakiwa katika umri wa barehe na ujanani wakati homoni kama za testosterone zinaongezeka mwilini. Wanawake hupata chunusi zaidi wanapofikia umri wa kuanza kupata siku za mwezi. Wanawake wengi huota chunusi siku chache kabla ya kuingia mwezini.
Kupunguza kunata kwa seli za ngozi zilizokufa ili ziliweze kutiririka kiurahisi na kutoka nje ya vijitundu vya kwenye ngozi. Lotion kama salicylic acid 2% zinaweza kutumika.