Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wa mataifa yote na wa umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata chunusi.
Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana na chunusi.
Katika mwili wa binadamu, chunusi huonekana zaidi maeneo ya usoni, mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni. Kutegemeana na uwingi wa chunusi hizo, mwathirika huweza kunyanyasika kimawazo na kupata makovu juu ya ngozi yake. Kuna dawa za kutibu chunusi ingawa ni ugonjwa unaoweza kujirudiarudia.

Chunusi huondoka polepole sana na wakati mwingine chunusi mpya huanza kujitokeza kabla nyingine kupona kabisa. Ni ugonjwa unaotakiwa kupewa tiba ya mapema ili kuepuka kupata madhara ya kudumu.
Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles). Picha hapa chini inaonyesha muundo wa kitengo kimoja cha kinyweleo (pilosebaceous unit).
Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.
Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.
Sebum hii iliyotengenezwa na sebacious gland huchanganyikana na seli za ngozi zilizokufa na kwa pamoja hutolewa nje ya mwili kupiti vijitundu vya vinyweleo. Vijindu hivi vikijaa mchanganyiko huo, humwaga ziada juu ya ngozi na na kuifanya kuwa laini. Hali hii ikiendelea bila dosari, ngozo hubaki laini na yenye afya.
Chunusi za aina mbalimbali hutokea pale kunapotokea dosari katika ufanyaji kazi wa vijitengo hivi vya kwenye ngozi. Tutaelezea dosari mabilimbali zinazoweza kutokea, na nini kitaonekana juu ya ngozi ya mtu huyu. Kuna dosari ambazo zitaleta vijipele vya kawaida na nyingine kuleta mapele makubwa, mara nyingine yaliyotunga usaha.
Aiseeh!DNA yako ni kiboko maana ina pizza na usingizi[emoji23][emoji23][emoji23]wewe utakuwa ni kibonge level ya mwisho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuongezeka kwa vitu hivi ndani ya kijitundu cha kinyweleo, huziba sehemu ya juu ya kijitundu na kuzuia vitu hivi visitoke nje, hali ambayo kiutaalamu huitwa microcomedone.
Bakteria waitwao Propionibacterium acnes, huishi ndani ya vijitundu hivi vya vinyweleo na hutumia sebum kama chakula chao. Kuongezeka kwa sebum hufanya bacteria hawa kuongezeka ndani ya vijitundu hivi lakini hawaleti madhara yo yote kwa sababu hadi sasa wanaishi ndani ya vijitundu tu – hawana madhara kwenye ngozi.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.