Malaria bado ni ishu na vifo vinazidi kuongezeka[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Wataalamu wa afya wameonya kuwa udhibiti wa ugonjwa wa malaria umekwama baada ya miaka kadhaa ya mafanikio, na wameonya kwamba kushindwa kuimarisha juhudi na ufadhili wa kupambana na ugonjwa huo huenda ukaongeza idadi ya vifo vitokanavyo na malaria na maambukizi. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema nchi nyingi zimeripoti kuongezeka kwa visa vya Malaria, hasa zile zenye mbu wengi. WHO iimesema kiasi ya watu milioni 216 waliugua malaria mwaka 2016. Visa milioni tano viliongezeka kwa mwaka huo ikilinganishwa na mwaka 2015. Kwa mujibu wa WHO, visa vingi vinatokea kwa watoto wadogo katika nchi masikini za kusini mwa jangwa la Sahara.