Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Akizungumza leo Desemba 3 mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Catherine Moshi alisema bomoabomoa hiyo ilihusisha vibanda vya stendi ya daladala ya Jamatini, vibanda vya stendi ya mbasi ya kwenda mikoani, Ofisi za kampuni ya mabasi ya Shabiby na Abc, Mgahawa wa Cape Town na kituo kimoja cha mafuta kilichokuwa karibu na ofisi za Shabiby.
 
Kuhusu stendi a mabasi, amesema wamekubaliana na uongozi wa mkoa na manispaa kuwapa muda wa kuondoa stendi mbili za mabasi yaendayo mkoani na ya daladala ya Jamatini.
 
Wamesema kuondoa stendi sasa italeta shida kwa hiyo kuna makubaliano ambayo tumekubaliana na Mkuu wa Mkoa (Dk Binilith Mahenge) wa kutoa muda wa wao kuzihamisha,”alisema.
 
Hata hivyo, alisema makubaliano yao si kwamba stendi hizo zinabaki bila kubomolewa bali ni kwa muda na ukiisha wawe wamepata eneo la kupeleka huduma hizo ili eneo libaki tupu likabidhiwe kwa mkandarasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…