Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. Basal Tears: Hii ni aina ya machozi ambayo huwezesha macho yetu kuwa na majimaji kila wakati ( lubiricating tears) na kufanya macho yaone vizuri
 
2. Reflex Tears: Haya ni machozi ambayo huweza kutoka pale kitu kinachowasha macho kama vile kitunguu, mabomu ya machozi huingia machoni.
 
3. Emotional Tears Hii ni aina ya machozi ambayo hutoka kutokana na kuguswa hisia, au tukuto moyoni.
 
Wana unyevunyevu wa kutosha kulinda macho yao, lakini machozi halisi huanza kutoka majuma kadhaa baada ya vifereji vyao vya machozi kukomaa kikamili.
 
MACHOZI YANAYOONDOA STRESS?
Wanasayansi wamegundua kwamba Emotional tears (aina ya tatu) huwa na kiwango kikubwa cha madini ya manganese na homoni za prolactin ambazo husaidia mliaji kujisikia ahueni baada ya kilio.
 
Ukweli asilimia 85 ya wanawake wanakiri kwamba baada ya kutoa machozi au kulia kujisikia relief na wapo relaxed.
 
Kulia (KUTOA MACHOZI) ni moja ya njia ya asili ya kuondoa stress ikiwa ni pamoja na kucheka, kutembea, kukimbia, kupiga kelele na pamoja na kufanya ishara mbalimbali. Je unaamini kwamba njia nzuri ya kuondoa stress ni mwili wako mwenyewe? INAKUWAJE? Tunapokuwa stressed miili yetu inajaa kemikali ambazo huweza kuharibu hisia na mood.
 
Baada ya kulia (kutoa machozi) mwili huweza kuondoa hizo kemikali kwa kupitia machozi. Unapotoa machozi huku upo emotional (hasira, stress, maumivu, umeudhika, umekwazwa, mawazo, umechoka nk) zaidi mwili huweza kutoa homoni za protein kama vile Leucine Enkephalin ( hii ni natural pain killer ), prolactin na adrenocorticotropic hizi hupunguza stress zaidi na kukufanya usijikia raha na ahueni.
 
JINSI YA KULIA AU KUTOA MACHOZI
Ukishaona una stress, au umekarisika au umeumizwa au una mawazo na unajisikia kutoa machozi au kulia, tafuta sehemu ambayo ni ya siri na peke yako, sehemu yenye utulivu harafu ruhusu kilio chenye machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye cheeks (mashavu),
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…