Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kulia (KUTOA MACHOZI) ni moja ya njia ya asili ya kuondoa stress ikiwa ni pamoja na kucheka, kutembea, kukimbia, kupiga kelele na pamoja na kufanya ishara mbalimbali. Je unaamini kwamba njia nzuri ya kuondoa stress ni mwili wako mwenyewe? INAKUWAJE? Tunapokuwa stressed miili yetu inajaa kemikali ambazo huweza kuharibu hisia na mood.
 
Baada ya kulia (kutoa machozi) mwili huweza kuondoa hizo kemikali kwa kupitia machozi. Unapotoa machozi huku upo emotional (hasira, stress, maumivu, umeudhika, umekwazwa, mawazo, umechoka nk) zaidi mwili huweza kutoa homoni za protein kama vile Leucine Enkephalin ( hii ni natural pain killer ), prolactin na adrenocorticotropic hizi hupunguza stress zaidi na kukufanya usijikia raha na ahueni.
 
JINSI YA KULIA AU KUTOA MACHOZI
Ukishaona una stress, au umekarisika au umeumizwa au una mawazo na unajisikia kutoa machozi au kulia, tafuta sehemu ambayo ni ya siri na peke yako, sehemu yenye utulivu harafu ruhusu kilio chenye machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye cheeks (mashavu),
 
hakikisha unaruhusu emotions zako za ndani kuhusika katika kulia kwako ili utoe machozi mengi na ya maana (content) kwani ni tiba bora zaidi na utajisikia bora zaidi na pia kujisikia kama umetua mzigo mzito ndani ya mwili wako.
 
Hii ina maana kwamba kama mtu (mume au mwanamke) anatoa machozi si vema kumzuia asilia badala yake mpe usiri au muda alie hadi achoke mwenyewe kwani hiyo ni dawa muhimu kwake. Baada ya kutoa machozi yako hakikisha unakuwa na mood nzuri kwani machozi pia husaidia kukuwezesha ku-clear Mind.
 
View attachment 646856
Haya makitu yanakukumbusha wapi?
Haya makitu mazuri sana (wenzio wameyabatiza eti ndo lugha ya Mungu) sema tu ufundishwaji wake ndo hovyo. Viboko vya mgongoni sana tu nilikuwa nanyukwa. Uonevu mtupu! Kuna kakitabu kanaitwa "Famous Mathematical Formulas Explained" yaani kanaeleza vizuri mpaka hata sisi vilaza tunaelewa kabisa.
 
Watu wengi wako kwenye uhusiano wa kimapenzi bila kujua kama kweli wanapenda kwa dhati au wanajilazimisha sasa Ili kutambua upendo wako jipime kwa maswali yafuatayo:
 
Unapoamka asubuhi wazo la kwanza kukujia linamhusu mpenzi wako au unafikiria zaidi kazi na mambo mengine? Una msukumo wa kutaka
kumsalimia na pengine kumuuliza anapenda afungue kinywa kwa chakula gani?
 
Je umekuwa mwepesi na mwenye furaha kubwa kuwaambia rafiki zako wa karibu juu ya hisia zako kwa mpenzi wako? Unajisikiaje wanapokushawishi vibaya kuhusu yeye?
 
Hebu jiulize ni mara ngapi umekuwa ukishawishika kumnunulia mpenzi
wako nguo, mapambo au vitu kwa lengo la kumfanya avutie au ndiyo
umemtelekeza na kumwacha aonekane mchafu na asiyevutia mbele za watu?
 
Tukisema Wivu katika mapenzi unamaanisha mtu kumiliki mpenzi wake peke yake pasipo kuingiliwa na mwingine, kwa maana nyingine kuonyesha unampenda na kumjali ila ukizidi unakuwa sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…