Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini kwa kiumbe kinachovuta pumzi lazima kiwe katika hali hiyo na kama huna huku bado unavuta pumzi basi hujui nini maana ya kupenda. Lakini kwa yeyote anayeijua thamani ya kupenda lazima atakuwa anajua maana ya wivu.
 
Wivu katika mapenzi ndiyo chachandu kwa mtu kujua kweli anapendwa. Huwezi kuwa na mke au mume akichelewa au kusimama mazingira yasiyo eleweka ukae kimya, ujue lazima kuna walakini akilini mwako.
 
Rangi zinaweza kuelezea tabia ya mvaaji kwa harakaharaka hata kama haumfahamu kama moja ya chapisho la jarida la Readers Digest linavyoeleza.

Tukianza na rangi Nyeupe
Rangi hii hubeba nadharia ya usafi. Humfanya mvaaji aonekane mtu anayependa usafi si wa mwili tu bali hata tabia kwa neno zuri ni ‘purity’.Pia rangi hii husimama sehemu nyingi, haichagua sehemu ya kuvaa.
 
Nyeusi
Watu wengi hupendelea nguo nyeusi. Rangi hii humpa mvaaji mwonekano wa kujiamini na jasiri, ndiyo maana watu wengi hupendelea kuvaa mavazi yenye rangi nyeusi wanapokwenda kwenye usaili wa kazi.
 
Njano
Ni rangi ambayo mtu akivaa anaonekana mwenye furaha wakati wote. Hata kama mtu ana huzuni na masononeko moyoni, akivaa nguo ya rangi hii humwelezea kuwa ni mtu wa furaha na anayependa kuwa na furaha siku zote.
 
Nyekundu
Hii ni rangi inayoonyesha nguvu na kwamba una uwezo wa kufanya chochote.Ukivaa nguo nyekundu hata katika mkusanyiko wa watu wengi mtu anaweza kupita. Hata kama hujiamini hiyo rangi itakuaminisha na ndivyo watu watakavyokuchukulia.
 
Bluu
Hii inakuonyesha umetulia, watu huwa na mawazo chanya na mtu anayevaa nguo yenye rangi ya bluu. Mvaaji anaonekana siyo mtu wa kutetereka na kwamba ana uwezo wa kukabiliana na jambo lolote. Pia rangi ya bluu huvaliwa sana kwenye usaili wa kazi.
 
Kijani
Rangi ya asili, mara nyingi inahusishwa na mazingira.Ukivaa nguo ya rangi ya kijani unaonekana mtu anayejali, mtunzaji na mpenda mazingira. Mtu anayedumisha asili, watu wengi wanaofuga rasta ‘marasta’ hupenda kuvaa nguo zenye rangi za kijani.
 
Zambarau
Zambarau inamwongelea mvaaji kama ni mtu mbunifu na mtu anayependa sana kuvaa, hapitwi nyuma na mitindo ya kisasa.

Kahawia
Unapovaa nguo ya rangi hii unaonekana mtu uliyetulia na mtu anaweza kukuamini hata pasi kukufahamu. Mtu asiyependa makuu, mtu watu.
 
Tatizo kubwa linalozuia watu wengi kudhibiti matumizi ya kipato ni tabia yao ya kufanya matumizi ya kujionyesha kwa watu, au kuigiza maisha ambayo hawana uwezo nayo.
 
Hili linaendelea kuwagharimu watu wengi sana, kama utaendelea kuishi maisha hayo kuwa na hakika utaendelea kuona kipato hakitoshi, na zaidi utaendelea kujikita katika madeni yasiona na umuhimu.
 
Tofauti iliyopo kati ya maskini na tajiri, ni namna wanavyofanya matumizi ya fedha zao. Maskini yeye hutumia kila fedha anayoipata lakini tajiri yeye hutumia kiasi cha fedha na kiasi huhifadhi kama akiba, na akiba hiyo, huwasaidia kuwekeza ili kutengeneza fedha nyingine zaidi.
 
Jifunze kutumia bajeti kuongoza matumizi yako.
Bajeti huwa ni muongozo wa matumizi yako katika kipindi fulani cha muda. Usipokuwa na bajeti, utakuwa kama mtu ambaye anabahatisha katika matumizi yake,
 
maana chochote kitakachoonekana mbele yake lazima kitamvutia na kukinunua. Utafiti unaonyesha kuwa aslimia zaidi ya 50, ya matumizi ya fedha za watu wa kawaida, huelekezwa katika matumizi ya vitu visivyo na umuhimu.
 
Tembea na fedha kidogo.
Jitahidi sna kujenga tabia ya kutembea na fedha kidogo, au fedha za kile unachokwenda kununua tu. Acha fedha nyingine nyumbani au jifunze kuweka fedha eneo ambalo si rahisi kulifikia kwa haraka. Hii itakusaidia kutokufanya yale matumizi ya shinikizo.
 
Jipe muda kidogo kabla ya kununua kitu.
Unapojipa muda zaidi wa siku hata moja kabla kufanya manunuzi ya kile ulichotaka kununua itakusaidia kujitathimini kweli kama ulichokihitaji kukinunua kina umuhimu wowote kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…