Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umemaliza.

Nikizionaga tu hazifunguki narudi shambani kupalilia maparachichi.
Network huku bila antenna ya Chadema[emoji111] haupati kitu.
Good morning watu wa Mungu[emoji120]
 
tafiti zilizofanywa na jarida la new england journal of medicine nchini uingereza limegundua kwamba zaidi ya watu milioni moja na laki sita wanauawa na na ulaji wa chumvi kila mwaka, kifo ni hatua ya mwisho ya madhara ya chumvi lakini kuna madhara mengi sana yasababishwao na chumvi kabla ya kifo.
 
kitaalamu chumvi ni kompaundi au mchanganyiko wa element za sodium chloride, kemikali hii hutumika kuhifadhi chakula na kuleta ladha ya chakula, kemikali hii huweka kiwango cha maji mwilini sawa na kusaidia utumaji wa taarifa kwenye mishipa ya fahamu,
 
husaidia kuhifadhi maji mwilini, ni muhimu kwenye damu ya mwili,kutengeneza tindikali kwa ajili ya mmengenyo wa chakula tumboni, hata dripi za maji tunazopewa mahospitalini hua zina chumvi.
maisha ya kisasa na vyakula viulivyopo vinawafanya watu kula chumvi nyingi sana kuliko zamani,
 
hii husababisha madhara makubwa ambayo hayatibiki kirahisi.
kiafya mtu anatakiwa ale chakula chenye chumvi inayosikika kwa mbali sana na asiongeze chumvi chakula kinapokua mezani, hii ni sawa na gramu 1.5 mpaka 2.3 kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chakula kwa siku nzima.
 
ulaji mkubwa wa chumvi kwa wakati mmoja husababisha kuishiwa maji kwa seli, hii huleta kuchanganyikiwa, degedege, kupoteza fahamu na kifo lakini pia uwepo wa chumvi kidogo sana kwenye damu husababisha kuvimba kwa seli, kuchanganyikiwa,kupoteza fahamu na kufa..hii hutokana na unywaji mkubwa wa maji kupitiliza kiasi kwa wakati mmoja.
 
kimsingi vyakula vingi tunavyokula vina chumvi ya kutosha ambayo inatosha kabisa kuendesha mwili wetu bila kuongeza chumvi nyingine ya ziada, vyakula hivyo ni kama vitunguu,malimao,maji ya kunywa,viazi,ngano,nyanya,maboga,caroti, spinachi, kabechi,mapera, zabibu,epo,karanga,mayai, maziwa na vingine vingi
 
yafuatayo ni madhara ya ulaji wa chumvi nyingi ambayo yanaweza kua ya muda mrefu au ya muda mfupi.
yafuatayo ni madhara ya muda mrefu wa kula chumvi nyingi kwenye chakula...
 
presha ya damu; chumvi ina tabia ya kuzuia maji kutoka nje ya mwili kupitia mkojo, lakini pia kuna ushahidi kwamba kupunguza ulaji wa chumvi kwa wagonjwa wa presha hupunguza presha kwa wagonjwa wa presha
 
kansa ya tumbo; utafiti umeonyesha kwamba nchi ambazo kuna ulaji mkibwa sana wa chumvi kama japani kuna wagonjwa wengi sana wa kansa ya tumbo la chakula ukilinganisha na nchi ambazo hazina ulaji mkubwa wa chumvi kama uingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…